Mar 18, 2014

CHIFU WA WANYIHA MWENE SHANTIWA MLOTWA AITAKA SERIKALI IWAACHIE MACHIFU KUADHIBU WAHALIBIFU WA MAZINGIRA


 Wajumbe waliohudhulia kwenye chanzo cha maji katika eneo la Halungu ambako mradi mkubwa wa maji utajengwa
 Mhandisi wa Maji Mbozi  Eckson Mwasyange akizungumza kwenye uwekaji jiwe la msingi
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Ambakisye akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Halungu
 Chifu Mlotwa Shantiwa akipanda mti kwenye uzinduzi wa mradi wa maji Halungu
 Wakuu wa idara na wakazi wa Halungu wakipanda miti katika chanzo cha maji Halungu
 Mwandishi wa TBC Hosea Cheyo akiongozana na chifu Mlotwa Shantiwa
 Diwani wa kata ya Halungu Mh Simkoko akizungumza na wakazi wa kijiji hicho juu ya mradi wa maji unaotarajiwa kutekelezwa

Wazee wa kinyakyusa wakiingia kwa mbwembwe kwenye Ling'oma



na Mwandishi wa Indaba Africa-Mbozi

Mwenyekiti wa baraza la machifu wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya Chifu Mlotwa Shantiwa ameitaka serikali kuachia baadhi ya mambo na hasa masuala ya adhabu kwamakosa ya  uhifadhi wa mazingira kwa mamlaka za kimila ili kuwezesha kujenga nidhamu katika jamii.

Akizungumza katika kijiji cha Halungu wilayani Mbozi, chifu huyo amesema sheria za kitaalam zimeonekana kushindwa kufanya kazi hasa kwenye uhifadhi wa vyanzo vya maji ambapo hali imeendelea kuwa mbaya licha ya sheria hizo kuwepo

Alisema ili kujenga nidhamu na kutia uoga katika jamii, ni vyema machifu wakaachiwa sehemu ya majukumu ya kuadhibu wanaoharibu mazingira ili kuwezesha vizazi vijavyo angalau kufaidi sehemu ya raslimali zilizopo

Aliyasema hayo wakati wa kuwekwa jiwe la msingi la mradi wa maji kwa vijiji vya Halungu na Sasenga vyenye zaidi ya wakazi 9,500, mradi ambao utagharimu jumla ya shilingi million 668 mpaka kukamilika kwake.

Mapema akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi  Erick Ambakisye  ameelezea kusikitishwa na ari ndogo ya uchangiaji asilimia 5% ya mradi ambapo katika kipindi cha miaka minne wananchi wamechangia shilingi million moja tu kati ya shilingi 32 milion walizopaswa kuchangia.

Alisema hali hiyo inaweza kukwamisha uwezekano wa fulsa zingine za miradi ya maendeleo kuelekezwa kwa wananchi hao.

Kulingana  na mhandisi wa maji wilaya ya Mbozi bwana Ackson Mwasyange, mradi  huo utaanza kutekelezwa mwezi April na unakusudiwa kukamilika mwezi March 2015, na kwamba ni miongoni mwa miradi mingine mitano inayotekelezwa wilayani Mbozi kwa kupitia program ya maji chini ya benki ya dunia.

Katika risala yao wananchi wa kijiji hicho wameonyesha kusikitishwa na ucheleweshaji wa mradi huo ambapo tangu mwaka 2004 serikali ilianzisha mchakato wa utekelezaji wa miradi hiyo mpaka sasa bado zimeendelea kutolewa taarifa za matumaini pasipo kupata huduma ya maji.

Mwisho