Kamishna
wa Tume ya kudhibiti UKIMWI TACAIDS Dk Violet Bakari ametahadharisha uwezekano wa kutokea vifo
zaidi na kutetereka kwa afya za watumiaji wa ARV ikiwa hawatapunguza matumizi ya pombe.
Alisema ingawa kwa
maeneo ya baridi baadhi ya watumiaji wa ARV wamekuwa wakisingizia hali ya
baridi kuchangia unywaji wa pombe, amesema vivyo hivyo kwa maeneo ya joto pia
imebainika watumiaji wa ARV wamekuwa watumiaji wa kileo hali ambayo amesema
isitumike kama kisingizio cha kuhalalisha kuathiri afya zao.
Amesema
uzoefu unaonyesha kadiri wanavyotumia dawa hizo na kuona afya zao zikiimarika,
ndivyo wengi wao walivyojiingiza kwenye matumizi ya pombe hali ambayo amesema
hawajatambua madhara yake kiafya na akawasihi afya zao zinazoimarika ziendane
na uzalishaji kwaajili kujiweka vyema kiuchumi.
Alisema
lengo la kuwawezesha kupata dawa hizo ni kuimarisha kinga zao na kuwawezesha
kutumia fulsa ya afya bora katika kuendelea kutoa mchango wao kwa taifa na
familia zao, tofauti na mtazamo wa wengi wao kuelekeza nguvu zao katika
matumizi makubwa ya pombe
Kwa
upande wake mkurugenzi wa tathmini na ufuatiliaji Dk Meshack Shimwela aliwataka
wananchi kutochagua njia moja ya kukabiliana na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Akijibu
maswali ya wananchi waliohoji muundo wa mipira ya kiume kutoziba sehemu kubwa
ya maeneo ya siri na matokeo yake kusababisha maji maji kutoka kwa mtu mmoja
kuhamia kwa mtu mwingine hivyo kuwepo hatari ya kuambukizana ikiwa mmoja
atakuwa na majeraha katika mwili.
Dk
Shimwela alisema, ni vyema wananchi wakatambua kuwa suala la matumizi ya
kondomu za kiume linafanyika pale watumiaji wanapokubaliana na huku wakiwa
timamu kiafya, lakini itakuwa maajabu kwa mtu kulazimisha kufanya mapenzi huku
akitambua anavidonda mwilini hali ambayo hawezi kulifurahia tendo hilo.
“ni
vyema tukatambua kuwa huduma tulizo nazo kila moja wapo hutumika kwa wakati, si
vyema tukalazimisha kila jambo lifanyike na huduma moja” alifafanua Dk Shimwela
Katika
ziara hiyo, tume imeridhishwa na utendaji wa afua za mapambano dhidi ya
UKIMWI ambapo watu wanaoishi na VVU
wamekuwa na miradi ya kiuchumi hali ambayo inapunguza unyanyapaa na ubaguzi
kwenye jamii wanazoishi. Takwimu za wilaya zinaonyesha kuna jumla ya wateja
11,500 walisajiliwa kutumia dawa za ARV katika wilaya ya Mbozi
MWISHO