Oct 15, 2014

ASHANTI MAJANGA" YAAMBULIA KICHAPO CHA 2 KAVU KUTOKA KIMONDO

Kikosi cha ASHANTI kilichoshuka dimbani dhidi ya Kimondo na kuambulia kichapo cha 2 Oclock

Hii ndiyo sumu ya Ashanti al maarufu kama Kimondo KISSC iliyoshuka jioni ya leo na kutoka na ushindi wa mabao matakatifu 2-0

Benchi la Kimondo


 Na Danny Tweve wa Indaba Africa,

 Ikicheza uwanja wake wa nyumbani Kimondo SSC ya Mbozi imeendelea kutunisha msuri kwa timu za maji ya chumvi , mara hii kwa kuibatua Ashanti United  mabao 2-0  kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliofanyika uwanja  wa  CCM Vwawa.
Hadi mapumziko , si Kimondo wala Ashanti walikuwa wamechungulia nyavu za timu pinzani licha ya Kimondo kukosa mabao matatu ya wazi katika gonga zilizochezwa kwenye lango la ASHANTI lakini papara za wachezaji wake ziliiharibu mabao hayo.
Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ya mfulizo yaliyofanywa na kocha wa timu ya Ashanti ambayo yaliongeza uhai na mashambuzi, gonga na viminyo vya hapa na pale, hata hivyo michezo ya kimjini mjini –zikiwemo rafu za hapa na pale, vipepsi na janja janja ziliwagharimu Ashanti  kwa wachezaji wake wawili kupewa kadi za njano kwa kuwajeruhi wachezaji wa kimondo ambao mmoja alishindwa kuendelea na mchezo.
Mnamo dakika ya 72 Kimondo kupitia kwa Michael  Mwailusu Bosco   baada  ya kutokea gonga nikugonge langoni mwa ASHANTI kufuatia kona iliyopigwa na Mshaki Simbeye
Dakika ya 89 Kimondo walitupia msumari wa moto langoni mwa Ashanti ulioenda moja kwa moja wavuni bila mlindamlango kuuona mpira ulioanzia wingi ya kushoto , bao lililofungwa na Geofrey Mwashuya ambaye katika mchezo huo alionekana wazi kuwa hatakuwa na timu ya Kimondo kwenye dirisha dogo la usajiri kutokana na  kiwango chake kuendelea kuvutia timu nyingi za ligi kuu.
Ama kwa upande wa mashabiki, burudani ya mchezo wa leo iliongezewa chachandu baada ya mashabiki wa  Mbeya City kukodi mabasi mawili kuja kuipa sapoti Kimondo ya Mbozi hali ambayo iliufanya uwanja ulindime kwa shamra shamra na mbwebwe za mashabiki hao.
Mchezo wa leo uliochezeshwa na mwamuzi Kinugani kutoka Morogoro akisaidiwa na Alphaxad Mteta kutoka Ruvuma, Cheyo kutoka songea , Kefa kayombo kutoka mbeya ulikuwa chini ya kamisaa  Zahra Mohamed mwamuzi wa siku nyingi wa michezo ya kimataifa.