Oct 19, 2014

MCHEZO WA KIMONDO NA KMC AMA TESSEMA WAVUNJIKA, NI BAADA YA UWANJA KUJAA MAJI


Kikosi cha TESSEMA  au Kinondoni Municipal Council kilichoshuka dimbani uwanja wa CCM Vwawa

Timu ya Kimondo ambayo marudio ya mchezo huo kesho wanapaswa kuyatumia vyema

waamuzi wa mchezo huo wakiwa na team captains wa timu zote mbili

Shabiki wa Kimondo akiogelea kwenye madimbwi ya uwanja huo baada ya mchezo kusimamishwa kutokana na maji kujaa

Meza ya mwamuzi ikiwa inaelea kwenye maji

Uwanja wa CCM Vwawa ukiwa umejaa maji


Mwendo wa Madimbwi uwanjani

Kamisaa wa mchezo huo Tinyendera akizungumza na viongozi wa timu zote kukubaliana kurejewa kwa mchezo huo hapo kesho majira ya saa nne asubuhi
  
NA MWANDISHI WA INDABA AFRICA
Mchezo wa ligi daraja la kwanza baina ta TESSEMA na Kimondo uliofanyika uwanja wa Vwawa CCM Mbozi umevunjia dakika ya 74 baada ya mvua kubwa iliyoanza kunyesha dakika ya 55 kuharibu starehe ya mchezo kwa kujaza maji uwanjani

Mchezo huo umevunjika TESSEMA ikiwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Moris Katumbo mnamo dakika ya 52 baada ya kumegewa pande zuri kutoka wingi ya kushoto lililosukumwa na Shabani Juma. Goli hili lilitokana na uzembe wa mmoja wa wachezaji wa Kimondo kuacha mpira akilalamikia mchezo mbaya uliofanywa na Ramadhan Choki, baada ya kona iliyopigwa na Mpoki Tauson wa Kimondo kuokolewa na walinzi wa TESSEMA.

Kosa hilo ambalo mwamuzi wa mchezo huo Hasan Abdalah  hakuliona liliwagharimu Kimondo baada ya kupenyezwa mpira mbele na kumkuta Shaban Juma ambaye alichungulia na kumtupia mfungaji.

Kwa ujumla kosa kosa nyingi kwa upande wa Kimondo zingeweza kuzaa lulu ya mabao katika mchezo huo, hata hivyo TESSEMA watapaswa kuwapongeza walinzi wao ambao walikuwa vidume kukabili mashambulizi ya wenyeji.

Kulingana na taratibu za TFF kwenye kanuni za ligi hiyo mchezo huo utaendelezwa  hapo kesho majira ya saa nne asubuhi kwakuwa dakika hazikuzidi 16.

Kanuni za TFF kwaajili ya ligi daraja la kwanza kifungu cha 3.(6) Kinaeleza kuwa  " Iwapo  mchezo  ulishaanza  na kuvunjika  kwa  sababu  ya  matukio  ya  dharura  yasiyotarajiwa wala kusababishwa na timu husika, utapangwa kurudiwa kwa muda  uliosalia,  magoli  yaliyofungwa na kadi zilizoonyeshwa  katika  mchezo huo zitaendelea kuhesabika".

Kwamazingira hayo Kesho kimondo inatakiwa kuyatumia mazingira hayo kuweka vyema rekodi yake ya uwanja wa nyumbani kwa kuhakikisha inapata mabao mawili katika kipindi cha dakika 15 ili kuondoa dosari ya bao moja walilolala nao jioni hii dhidi ya TESSEMA