Oct 24, 2014

KOZI YA MAKOCHA YAANZA LEO



Release No. 164
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 23, 2014

RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA
Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi ya makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Hafla ya ufungaji kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kozi hiyo ya wiki mbili iliyoanza Oktoba 12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.

Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).

Wengine ni Edna Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).

Pia wapo Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).

Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa vyeti vya ushiriki tu.  

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)