Release No. 164
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 23, 2014
RAIS
WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA
Rais wa Kamati
ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi
ya makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Hafla ya
ufungaji kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar
na kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF
zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kozi hiyo ya
wiki mbili iliyoanza Oktoba 12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.
Makocha
walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi),
Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe
(Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari
Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).
Wengine ni Edna
Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo
(Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said
(TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil
(Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
Pia wapo
Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina
(Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel
Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf
Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).
Makocha
watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa
vyeti vya ushiriki tu.
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)