Jan 29, 2014
MZEE ANAPOTOA BURUDANI
MZEE HUYU AMBAYE NI MKEREKETWA WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKAZI WA ENEO LA MAKUNGURU JIJINI MBEYA AKIWA NA ZANA ZA ASILI ZA MZIKI KATIKA MOJA YA SHUGHULI ZA KISERIKALI
UBORESHAJI HUDUMA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE WAZIDI KUIMARISHWA
MENEJA UENDESHAJI NA MASOKO BWANA KYOMO AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WAHABARI KUHUSIANA NA KUKODISHA COUNTER YA VINYWAJI UWANJA WA NDEGE SONGWE
HII NDIYO MIN BAR ILIYOPO UWANJA WA NDEGE AMBAYO IMEPATA MWEKEZAJI ATAKAYETOA HUDUMA UWANJANI HAPO
HII NDIYO MIN BAR ILIYOPO UWANJA WA NDEGE AMBAYO IMEPATA MWEKEZAJI ATAKAYETOA HUDUMA UWANJANI HAPO
Jan 27, 2014
TETE ATETE CONVERSATION
TETE ATETE CONVERSATION- wanaonekana wakinong'ona maneno ni Mpiga picha wa Raisi Bwana Fred Maro akiteta jambo na Bwana Joseph Mwaisango Mpigapicha na mhariri wa Mtandao wa kijamii wa Mbeya Yetu.
ENZI ZA SOMO LA SIASA SIKUMBUKI KUFUNDISHWA BENDERA HII
Ninaamini kuna hatua zimechukuliwa katika ufundishaji kwa shule za msingi, kwani wakati huo tukisoma somo la siasa sikuwahi kufundishwa juu ya bendera ya rais, zaidi ya bendera ya CCM wakati ule na ile ya Taifa, lakini katika makuzi nikaja kukutana na bendera hii na katika uliza uliza nikaambiwa ni bendera ya Rais
MCHELE WA SUMBAWANGA HUOOO
HUU NDIYO MCHELE WA SUMBAWANGA AMBAO KWA SASA UNAUFUKUZIA ULE WA KYELA KWA UBORA NA HASA AROMA YAKE!
FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY YAFURAHISHWA NA UTENDAJI WA ASASI ZINACHOCHIPUKIA
Bodi ya shirika la Foundation for Civil Society nchini ilipotembelea asasi ya Mbozi Society for HIV Campaign and Social Development wakiwa wamepozi kwa picha ya pamoja nje ya jengo la SELFINA zilimo ofisi za asasi hiyo wilayani Mbozi
Jan 26, 2014
mbozi yajipanga kukabiliana na uhaba wa madarasa
watendaji kata katika wilaya ya Mbozi wakiwa kwenye kikao cha kikazi kwaajili ya kutoa taarifa ya hali ya madarasa kwaaajili ya kuanza kidato cha kwanza
Afisa Mipango wilaya ya Mbozi bwana Elisey Ngoi akifafanua jambo kwenye kikao hicho
Afisa Mipango wilaya ya Mbozi bwana Elisey Ngoi akifafanua jambo kwenye kikao hicho
KUMBE NDEGE PIA ZINA NJIA ZAKE HUKO ANGANI?
HAPA NI UWANJA WA SONGWE, MENEJA KITENGO CHA KUONGOZA NDEGE WA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE AKIONYESHA NJIA ZA NDEGE ANGANI
GAZETI LA MFANYAKAZI LILILOZINDULIWA KWA MBWEMBWE ZOTE LIMEISHIA WAPI?
Awali nilikuwa nalipata kwenye mazingira yangu ya kazi, lakini sasa hivi halionekani mtaani kunani Mfanyakazi news paper? tena lilizinduliwa na mh Rais MEI MOSI ya mwaka 2013 miezi michache limepotea huku kwetu vijijini
VYAKULA MBADALA KWAWATU WANAOISHI NA VVU
BAADHI YA VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI MBOZI WAKIPIGWA SOMO NA ASASI YA MBOZI SOCIETY FOR HIV CAMPAIGN AND SOCIAL DEVELOPMENT JUU YA LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VVU
DALILI ZA MKOA WA SONGWE KUTANGAZWA ZIPO KARIBU IMEFAHAMIKA
NANI ALIJUA? ZIARAYA HUYU DR MKOA WA MBEYA ALIPOREJEA AKAWA WAZIRI KAMILI!!!!
Dkt SEIF SELEMAN RASHID akisalimiana na Dkt Charles Mkombachepa, kaimu mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Mbozi, na mara baada ya ziara hii na kurejea jijini Dar es salaam kama naibu waziri wa wizara ya afya, Mh Seif Seleman Rashid aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa wizara hiyo!! je ni matokeo ya yale maneno aliyotamkiwa ya baraka akiwa mbozi????
akisalimiana na afisa Utawala na raslimali watu wilaya ya Mbozi bwana Zabron Lulandala
Akipeana mkono na Hamis Mtoni Majani mratibu wa Tasaf wilaya ya Mbozi
Tabasamu hili alilitoa baada ya mmoja wa wajumbe kumtamkia wazi kuwa ziara hiyo inaweza kuwa ya baraka kwa mheshimiwa waziri atakaporejea jijini Dar es salaam hasa baada ya mengi aliyoelezwa kuonekana kuyapa uzito kwenye uimarishaji wa sekta ya afya nchini!
akisalimiana na afisa Utawala na raslimali watu wilaya ya Mbozi bwana Zabron Lulandala
Akipeana mkono na Hamis Mtoni Majani mratibu wa Tasaf wilaya ya Mbozi
Tabasamu hili alilitoa baada ya mmoja wa wajumbe kumtamkia wazi kuwa ziara hiyo inaweza kuwa ya baraka kwa mheshimiwa waziri atakaporejea jijini Dar es salaam hasa baada ya mengi aliyoelezwa kuonekana kuyapa uzito kwenye uimarishaji wa sekta ya afya nchini!
Jan 25, 2014
ZAMBI APOKELEWA KWA SHANGWE JIMBONI MBOZI, AAHIDI KUTOELEKEZA MAKOMBORA KWA WATUMISHI!
Mmoja wa makada wa CCM wilayani Mbozi Bwana Ndisana akikumbatiana na Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mh Godfrey Zambi baada ya kupokelewa katika mpaka wa Mbeya na Mbozi leo mchana
Wakazi wa Vwawa na vitongoji vyake waliojitokeza kumpokea mbunge wao baada ya kuteuiliwa kuwa naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
WanaCCM nao hawakuficha sura kwenye shughuli hii walijipambanua kwa chama chao kuwakilishwa na mwenyekiti wa mkoa wa mbeya kwenye uongozi wa wizara muhimu inayogusa maisha ya watanzania kila siku
Mh Zambi akiwasili eneo la mapokezi mpakani mwa wilaya ya Mbozi na Mbeya
Wadau mbalimbali walikuwepo kwenye tukio hilo la mapokezi
Madiwani pia walikuwa miongoni mwa walioshiriki kwenye mapokezi hayo, hapa ni bwana Kasebele akikumbatiana na mbunge wake
Katibu Tarafa ya Vwawa Bi Kasunga akisalimiana na Mh Zambi
Afisa Mipango halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Ngoi Elisey akisalimiana na naibu waziri mara baada ya kupokelewa katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Mbozi na kusomewa taarifa ya maendeleo ya wilaya
Hapa mheshimiwa Zambi akiwa na Mbunge wa Nkasi jukwaani
Zambi akimtambulisha mkewe kwenye mkutano ulioandaliwa na chama cha mapinduzi nje ya ofisi za chama za wilaya ya Mbozi
Na Danny Tweve Mbozi
Naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika amewatoa hofu watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi kuwa hana mpango wa kuwashushia makombora na kuwaandama baada ya kuteuliwa nafasi ya Naibu waziri wa kilimo, chakula na ushirika
Akizungumza wakati akipokea taarifa ya wilaya ya Mbozi katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mbozi, Bwana Zambi amesema, amepokea taarifa kuwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi wamejazwa hofu baada ya uteuzi wake na kwamba ana mpango wa kuwang'oa na kuwashughulikia baadhi ya watumishi
"nimesikia kuwa eti nina orodha ya watumishi ninaokusudia kuwashughulikia hapa halmashauri, naomba niwatoeni wasiwasi endeleeni kuchapa kazi, sitatumia madaraka yangu niliyopewa na raisi kuwaandama watumishi wa halmashauri hata kidogo" alieleza mheshimiwa zambi
Alisema hali hii ya kuwajaza hofu watumishi, pia imejitokeza kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wamekuwa wakishambulia uteuzi huo kuwa unatamsababishia Zambi asionekane jimboni, jambo ambalo amelifafanua kuwa, majukumu ya Naibu waziri yatamwezesha kuonana kwa karibu na wananchi kwakuwa wanapewa muda mara nne kwenye kipindi cha mwaka kurejea majimboni mwao
Jan 22, 2014
KWAHERI CHILEWA KWENYE UTUMISHI WA UMMA- MBOZI WASEMA UMETIMIZA ENEO LAKO!
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Daktari Charles Mkombachepa kwenye hafla ya kumuaga bwana Chilewa
Mshereheshaji bwana Msokwa akianzisha shughuli hiyo katika ukumbi wa Cathoric Centre Mkonongo
Mkuu wa mkoa wakichart chambo na Bwana Chilewa kushoto kwa mkuu wa mkoa ni mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk. Kadeghe
Kaimu Mkurugenzi Daktari Charles Mkombachepa akitoa neno kabla ya mambo kuchanganya kwenye sherehe hiyo
Waheshimiwa madiwani wakipunga mkono wa kwaheri kwa aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuiwezesha mbozi kupandisha mapato yake ya ndani kutoka milion 400 alifohamia mwaka 2006 hadi kufikia Bilion 3 anapoondoka
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Minga akizungumza jambo kwenye hafla hiyo ambapo alieza kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kukumbuka alama za maendeleo zilizoasisiwa na Bwana Chilewa ikiwemo miradi inayoendelea kutoa huduma kwa wananchi wake zikiwemo kituo cha mabasi cha Vwawa, Uanzishaji wa mamlaka ya mji wa Tunduma, mgawanyo wa wilaya ya Mbozi na kupata wilaya ya Momba na uimarishaji wa huduma za jamii hasa miundombinu, barabara , mawasiliano na michezo pia
Kitu kilijibu! hapa Hamisi Mtoni Majani mratibu wa TASAF Mbozi na Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Wakili msomi Deogratius Nchimbi wakizibua shampeni
Wakuu wa idara wakipanda kwa kwaito wakiongozwa na Kitashu the great" meneja mamlaka ya maji mji wa Vwawa
Watumishi wa idara ya afya nao wakatoka na jamii ya ndombolo !!
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakaingia na staili ya kunyemelea !!!
Mtendaji wa Mtandao wa Indaba africa alikuwemo pia
Kaimu katibu Tawala Mkoa Bwana Magacha alikumbushia maisha yake ya Mbozi na hatimaye ushirikiano alioupata hadi alipoteuliwa kuwa Afisa Tawala Mkoani
Ilikuwa ni furaha kwa Bwana na Bibi Chilewa baada ya kubaini watu wamejitokeza wengi kumuaga ikiwa ni dalili ya maisha aliyoishi na wakazi wa wilaya ya Mbozi yalikubalika
Mwenyekiti akaanzisha kusakata lumba
Timu ya madiwani ikielekea kumpa mkono wa kwaheri bwana Chilewa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi bwana Erick Minga akipeana mikono na bwana Chilewa ya kwaheri
Bwana Rashid Mbegu Moja ambaye alikuwa District Treasury akiagana na mama Chilewa, hata yeye pia baada ya siku chache akapata uhamisho
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Kandoro akitoa salam zake
shughuli ilimalizika kwa Msosi