Maji ya Nazi ni kinywaji kinachojitokeza ndani ya nazi mbichi almaarufu kama dafu ambayo huwa rangi ya kijani. Maji hayo huwa na kiwango cha mafuta 0, cholesterol 0 na ni chini ya kalori. Faida
kuu ya maji ya nazi ni kwamba maji haya yana kiwango kikubwa cha electrolytes kuzalisha kiwango cha upozaji mwili kwa siku nzima katika mazingira ya joto hata baada ya kuyanywa kwa muda mrefu hadi usiku wakati mwingine huendelea kupoza mwili.
Maji ya dafu yana madini ya Potasium zaidi kuliko ndizi, na mara 15 kiasi kinachopatikana katika vinywaji vya asili vingine. Potasiamu husaidia kuzuia kunywea kwa misuli.
Baadhi
ya makampuni ya maji ya nazi huongeza juisi kwa ladha ya bidhaa zao,
ambazo zinaweza kusababisha sukari nyingi na kalori, hivyo utahitaji
kuepuka hilo, lakini maji safi ya nazi ni mbadala nzuri ya vinywaji vinavyoweza kutumika
michezoni badala ya matumizi ya vinywaji bandia ama vya viwandani na vinywaji vingine vya sukari.
Sep 12, 2018
Jun 4, 2018
BENKI YA NMB YAJIELEKEZA KUJENGA UWEZO KWA VIKUNDI
Benki ya NMB Tawi la Mbozi na Mlowo kwa pamoja wameelezea nia yao ya kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Mbozi katika kushughulikia changamoto za ukuaji na uaminifu kwa vikundi vya wakulima ili mikopo inayopatikana iwe na tija kiuchumi
Wakizungumza na menejimenti na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Timu ya wataalamu wa benki hiyo wamesema bado jamii ya wananchi wa Mbozi hawajafikiwa vyema na elimu ya Mikopo kiwango ambacho wengi wa wanaojitokeza kukopa kutokujipanga vyema kulingana na mipango yao.
Wamesema ikiwa halmashauri inaona vyema kutoa huduma zake kupitia vikundi ni vyema wakaishirikisha benki hiyo ili kujenga uwezo na kuandaa wajasiliamali wenye nia ya dhati ya kujikwamua na umaskini kwanza badala ya kuanzisha programu za hamasa juu ya mikopo mbalimbali bila kuwaandaa kwanza
VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA VINGI VYAVUKA KIKWAZO KWENYE VIGEZO 2017/2018
Vituo vya kutolea huduma za afya 19 tu kati ya 80 ndivyo vilivyopata nyota sifuri katika tathmini ya mwaka 2017/2018 imefahamishwa.
Wakitoa taarifa ya ukaguzi wa hali ya vituo hivyo kwa kuzingatia mwongozo wa BRN, Wakaguzi wa wizara ya Afya wamesema kuna ongezeko kubwa la vituo vilivyovuka kutoka nyota sifuri hadi kuingia kwenye nyota moja ikilinganishwa na mwaka 2016.
Kwa mwaka 2016 vituo 45 vilipata nyota 0 kati yake vikiwemo zahanati 45 lakini kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti ambapo Zahanati 19 kati yake 16 za serikali zimepata nyota sifuri, zahanati 48 zimepata nyota moja, 8 Nyota Mbili ambapo vimo vituo vya afya na Hospitali ya Misheini ya Mbozi na Hospitali ya wilaya ya Mbozi imepata Nyota tatu.
Katika mchanganuo huo Zahanati ya Mbaya ambayo ni Binafsi imeshika nafasi ya mwisho kwa kupata wastani wa alama 0.
Katika uchambuzi huo miongoni mwa mapungufu yaliyobainishwa nipamoja na vituo 63 kati ya 80 kutokuwa na vyoo seti tatu kama mwongozo unavyotaka ambapo inashauriwa kuwa na vyoo vya wanawake, wanaume na watoa huduma (wataalamu) kwenye majengo ya zahanati, aidha kukosekana kwa vyoo rafiki kwaajili ya walemavu na wenye mahitaji maalumu.
Katika ukaguzi huo kulikuwa na jumla ya Maeneo 12 yaliyowekwa kwenye makundi katika ukaguzi yakiangalia uwezo na uendeshaji wa vituo vyenyewe ikiwa ni pamoja na miundombinu yake, utendaji wa wataalamu, Matumizi ya zana, vitendanishi na takwimu za afya zilizopo kituoni katika kupanga mipango ya mbele, ushughulikiaji wa huduma za dharura, mtazamo wa kumlenga mteja na uwajibikaji.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI YAJIELEKEZA KUFIKIA 100% YA MAKUSANYO
Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imeagizwa kusimamia ukusanyaji wa mapato yake ya ndani kwa asilimia 100, ili iweze kutekeleza miradi yake iliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi akiwa na wajumbe wenzake wa kamati ya Fedha ya Halmashauri hiyo ametoa msimamo wa madiwani wakati akizungumza na wananchi kata ya Isansa baada ya kamati hiyo kujiridhisha na ujenzi wa kituo cha afya unaofanywa kwa njia ya Force account.
Amesema wakati zimesalia siku chache kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha 2017/2018 ni vyema wataalamu wakatambua kuwa Halmashauri ya wilaya haijafanikiwa kutekeleza baadhi ya miradi ya Maendeleo kutokana na mapato kidogo ya ndani ambapo hadi kufikia Juni Mosi Halmashauri imefikia asilimia 78 ya makusanyo yake ya ndani hata hivyo kuna vyanzo vingi zikiwemo leseni za biashara ambazo bado hazijaweza kukusanywa vyema, hivyo mkakati wake kwa sasa ni kujielekeza kukusanya kwenye vyanzo hivyo sambamba na mazao baada ya msimu wa mavuno kuanza.
Kutokana na hatua hizo tayari timu ya mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi imeundwa ikihusisha wataalamu wa idara mbalimbali, huku kamati ya fedha ya Halmashauri hiyo ikikasimiwa majukumu ya kusimamia utendaji wa menejimenti katika kipindi chote ili kuhakikisha kuwa malengo yanafikiwa.
Kwa upande wao wataalamu wameahidi kutekeleza wajibu wao hasa katika suala la makusanyo na kwamba matarajio yao ni kuona kuwa Halmashauri yao inafanya vyema katika utekelezaji wa malengo yake ikiwemo miradi iliyopangwa.

May 29, 2018
DAWA YA KINGA YA VVU KULENGA MAKUNDI MAALUM
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo Mfuko wa Henry Jackson kutoka serikali ya Marekani wamo kwenye hatua za maandalizi kwaajili ya kutekeleza mpango wa utoaji dawa kinga kwa watu walio katika makundi maalumu ya jamii ambayo yapo kwenye hatari ya kuambukizwa.
Kulingana na taarifa za utekelezaji wa Mpango huo, wanawake wanaouza ngono pamoja na wanaume walio kwenye biashara hiyo watashiriki kwenye mpango huo baada ya hatua za awali ambapo watahamasishwa kujipima wenyewe na ikithibitika wana maambukizi wataunganishwa na huduma za CTC ikiwa ni pamoja na kuingizwa kwenye mpango wa matumizi ya dawa za kupunguza makali ARV's
Ama kwa upande mwingine wale ambao hawatakutwa na maambukizi, wataanza kutumia dawa kinga ambapo kila siku watawajibika kumeza kidonge kimoja kwa kipindi kinachofikia siku 21 mfululizo huku pia wakitumia njia za kinga zingine zinazoelekezwa kitaalamu. Hatua hiyo inalenga kupunguza uwezekano wa mtumiaji wa dawa kinga kuambukizwa na virusi ikiwa ataacha kutumia njia zingine ikiwemo matumizi ya Kondomu katika kipindi cha matazamio ya dawa.
Kutokana na takwimu kuonyesha nchini Tanzania asilimia 25 ya wanawake wanaouza ngono wamo kwenye hatari ya maambukizi na katika utafiti uliofanyika hivi karibuni walibainika kuwa na maambukizi ya VVU, wakati ambapo 26% wanaume wanaofanya ngono ya wanaume kwa wanaume pia walibainika kuwa na maambukizi wakati 36% ya wanaotumia dawa za kulevya pia walikutwa na maambukizi hayo.
Mpango huo utatekelezwa kwenye vituo vya afya vyenye huduma za CTC,kwa kuzingatia idadi ya wateja wanaotumia ARV's, Uwepo wa wataalamu waliopata mafunzo ya utoaji huduma kwa watu wanaoishi na VVU.
Kutokana na utaratibu huo si kila Mtanzania atafikiwa na Dawa Kinga hiyo hivyo imesisitizwa umuhimu wa watanzania kuendelea kutumia njia za kinga zilizoelekezwa na wataalamu ili hatua ya majaribio ya dawa Kinga ya sasa yaweze kupimwa kwenye kundi lengwa la wanaouza ngono kwa baadhi ya maeneo yaliyoingizwa kwenye mpango huo katika Mkoa wa Mbeya na Songwe.

UMISETA MOTO- SONGWE YAKOLEZA JIKO KUTETEA UBINGWA TAIFA
Timu ya Umoja wa wanafunzi wa Sekondari -Mkoa wa Songwe, imo kwenye hatua za mwisho kwenda kushiriki mashindano ya Taifa yanayokusudiwa kufanyika Mkoani Mwanza. Timu hiyo imeundwa rasmi na orodha ya wachezaji kusomwa mbele ya afisa elimu Mkoa wa Songwe JUMA MHINA juzi katika uwanja waa shule ya sekondari ya Vwawa.
Timu hiyo yenye wachezaji 120 itawakilisha mkoa wa Songwe katika michezo ya Mpira wa Miguu kwa wanaume, Mpira wa Pete, Riadha, Mpira wa mikono, Mpira wa Kikapu na michezo ya ndani.Mkoa wa Songwe ndiyo bingwa wa taifa ka mwaka uliopita ambapo iliweza kuwadungua Unguja kwenye mpira wa Miguu katika fainali.