TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI KUHUSU MATOKEO YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI
(HBS) TANZANIA BARA 2011/12, TAREHE 14 NOVEMBA, 2013
Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Wizara ya Fedha iliendesha Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara
katika mwaka 2011/12. Utafiti huu ulikusanya,
kuandaa na kuchambua taarifa za mapato, matumizi na manunuzi ya kaya
Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2011/12 umelenga kutoa viashiria vitakavyosaidia kufuatilia na
kutathmini maendeleo ya sekta mbalimbali
zilizoainishwa kwenye Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II)
Tanzania.
Takwimu zilizokusanywa zilihusu watu na kaya katika maeneo yafuatayo:
Elimu na afya ya Wanakaya;
Manunuzi na matumizi ya kaya;
Umiliki wa vifaa na rasilimali;
Makazi na vifaa vya ujenzi;
Upatikanaji wa huduma na vifaa;
Upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira;
Shughuli za kiuchumi na ajira;
Utalii;
Umiliki wa biashara zisizo za kilimo; na
Shughuli za kilimo.
Utafiti huu ulifanyika kuanzia mwezi
Oktoba 2011 hadi Oktoba 2012 ambapo jumla ya kaya 10,186
kati ya 10,400 zilizokuwa zimelengwa zilihojiwa kutoka katika maeneo ya Dar es Salaam, maeneo
mengine ya mjini na vijijini, Tanzania
Bara.
Kila kaya iliyochaguliwa ilihojiwa juu ya masuala yote yaliyotajwa hapo
juu pamoja na kujaza kijitabu
cha kumbukumbu ambacho kaya ilitakiwa kuandika mapato na matumizi ya kila siku kwa muda wa siku 28 mfululizo. Kijitabu hiki cha
kumbukumbu kililenga katika kupata
matumizi ya moja kwa moja (hasa chakula)
ya kaya pamoja na matumizi mengine yasiyo ya chakula kwa kipindi hicho cha siku 28.
Matokeo ya utafiti huu
yanaonesha kuwa kiwango cha umaskini wa chakula na ule wa
mahitaji ya msingi ni tatizo zaidi
kwa Wananchi wa vijijini ikilinganishwa
na Wananchi wanaoishi mjini hususan Dar es Salaam na maeneo mengine ya mjini.
Wakati wastani wa kitaifa wa kiwango cha umaskini wa chakula ni asilimia 9.7,
kiwango hicho kinafikia asilimia
11.3 kwa maeneo ya vijijini.
Dar es Salaam ina kiwango
cha chini kabisa cha umaskini wa chakula cha asilimia 1.0 ambapo
Wananchi anaoishi maeneo mengine
ya mjini wana umaskini wa chakula wa asilimia 8.7.
Kwa upande wa umaskini wa mahitaji ya msingi, wastani wa Tanzania Bara ni asilimia 28.2 kilinganishwa na asilimia 33.3 kwa maeneo ya vijijini na asilimia 21.7 kwa
maeneo mengine ya mjini. Dar es Salaam
ina kiwango cha chini cha umaskini wa mahitaji
ya msingi cha asilimia 4.1.
Matokeo ya utafiti huu yanaonesha jitihada za Serikali katika kuongeza ujenzi wa
shule zaidi hasa
zile za sekondari ambazo zimewezesha kupanda kwa kiwango cha wanafunzi wanaojiunga katika elimu ya
sekondari kwa karibu mara mbili, kutoka asilimia 15 mwaka
2007 hadi asilimia 29 mwaka 2011/12.
Matumizi ya nishati ya umeme katika maisha ya kila siku ya Wananchi katika kaya ni eneo lingine ambalo
Serikali imelenga kuliboresha katika jitahada zake za kuboresha maisha ya Wananchi. Matokeo ya utafiti huu
yanaonesha kuwa kaya zinazotumia umeme angalau kwa ajili ya
mwangaza wa ndani zimeongezeka kutoka
asilimia 13 kwa mwaka 2007 hadi asilimia
18 kwa mwaka 2011/12