Naibu waziri wa Elimu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbozi Godfrey Zambi siku alipofika wilayani Mbozi, wilaya ya Mbozi imo kwenye mchakato wa kupata mkoa wake
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dr Kadeghe akimtambulisha naibu waziri kwa kaimu Mkurugenzi Mbozi Dr Charles Mkombachepa
Walimu wakimsikiliza naibu waziri
walimu wakifuatilia majadiliano
May 29, 2013
May 28, 2013
MGAWANYO WA MKOA WA MBEYA WAJIELEKEZA KUVUTIA KIMAKABILA
Na Mwandishi wa Indaba Africa,
Mnyukano wa ugawaji
wa mkoa wa Mbeya umeendelea kujenga sura ya uasilia wa waliopo kwenye madaraka
kutokana na wanasiasa kuvutia maeneo walikotoka bila kujali vigezo vya msingi
ikiwemo idadi ya watu.
Kulingana na vikao
vinavyoendelea, wilaya ya Rungwe tayari imeshajitengenezea mazingira mazuri ya
kupigiwa debe kuwa mkoa kwa kile kinachobainishwa kuwa madiwani wengi katika
mkoa wa Mbeya asili yao ni wilaya ya Rungwe
Dhana ya “kumitu
kukhaja ” inaonekana wazi wakati huu
kwenye mchakato wa kutoa mapendekezo ya wapi na maeneo yapi yaunganishwe
kuunda mkoa wa mpya baada ya Mh Rais
Kikwete kutamka wazi na kubariki mchakato huo wakati wa maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi mei mosi.
Mfano wa kujipigia
debe unaonyesha kuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbarali Keneth Ndingo ni
mkazi wa Rungwe hivyo maamuzi ya baraza la madiwani la Mbarali yanaonekana kuwa
na msukumo wa nyumbani, ambapo wamependekeza makao makuu yawe Rungwe
Maajabu ya musa
yanajitokeza katika ugawaji unaopendekezwa ambapo inaelezwa kuwa Mbarali
wanapendekeza halmashauri za Busokelo, Rungwe, Kyela, Ileje na Mbozi ziunde
mkoa mpya wakati kijiografia havina uwiano kati ya Mbozi na Rungwe.
Kulingana na takwimu
za sense ya mwaka2012, wilaya ya Mbozi kabla ya kugawanywa kupata Momba ilikuwa
na wakazi 740,719 idadi ambayo ni sawa na idadi za wakazi wa wilaya za Kyela,
Rungwe na Ileje ambazo kwa pamoja ni wakazi 685,098 hivyo kuwepo kwa pengo la
55621 zaidi kwa upande wa Mbozi
Kulingana na
jiografia ya mkoa wa Mbeya, Mkoa ambao kwa sasa ungeweza kuundwa kwa
kuunganisha wilaya za Ileje, Mbozi,
Momba na sehemu ya wilaya ya Chunya (jimbo la Songwe) ambalo limejitenga na eneo
la Lupa kwa umbali wake.
Kwa takwimu hizo hizo
mkoa wa huo ungeweza kuwa na idadi ya
wakazi 1,201,327 ambao ni asilimia 44.4
ya takwimu za sasa za wakazi wa mkoa wa Mbeya wanaofikia 2,707,410.
Ingawa jitihada za
kujipanga zimeanza kwa upande wa wilaya za Rungwe, Mbarali na Kyela kwa kufanya
ushawishi wa mbinu,ukweli unabakia kuwa wilaya ya Mbozi peke yake inavigezo
vyote vya kupata mkoa mpya kuanzia idadi ya watu, eneo la utawala,makazi, uwezo
wa raslimali za ndani kujiendesha na fulsa za kiuchumi zilizopo na zinazoweza
kupatikana.
May 27, 2013
KIMONDO YAANZA RAUNDI YA PILI YA MABINGWA WA MIKOA KWA KUTOA KICHAPO CHA BEBERU JIZI!
Timu ya Kimondo SC ya
wilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya imeendelea kutakata katika raundi ya pili
ya ligi ya Mabingwa wa Mikoa baadaya kuisukutua bila dawa timu ya Mji ya Njombe
bao 1-0 juzi katika mchezo uliofanyika uwanja wa sabasaba mjini Njombe
Katika mchezo huo ambao
tangu kuanza kwake ulikuwa ukionyesha jitihada za wazi za kuhitajika mbeleko
kwa timu ya wenyeji, hali iliendelea kuwa tete kadiri dakika zilivyokuwa
zikienda mbele kutokana na mbinu za hapa na pale za mwamuzi kushindwa kupenya
ili kuleta madhara kwa upande wa Kimondo.
Kimondo licha ya majaribio
kadhaa vipyenga vya kuotea vilionekana kuharibu ladha ya mchezo kiasi cha
mashabiki wa Njombe kushindwa uzalendo na kuamua kushabikia timu ya Kimondo
ambayo ilionekana kutandaza soka lenye ladha mithiri ya asali ya Ilomba na
Idiwili.
Katika dakika za mkiani,
baada ya majaribio kadhaa ya kuingia eneo la hatari na kupigiwa vipyenga vya
kuotea, ndipo staili ya “mpime huko huko mbali” ilipoanza na haikuchukua muda
mrefu kwani gonga kama nne kutoka kwenye lango la Kimondo zikielekezwa kwenye
lango la timu ya Mji Njombe ziliwezesha shuti la umbali wa mita 52.56 kuleta sherehe kwa upande wa Kimondo baada ya
kumpima kipa wa Mji Njombe na katika maeneo hatarishi na kusababisha timu
ipumulie mashine mbele ya mashabiki wake uwanja wa nyumbani.
Ushindi huo ulipakatwa kama
mwali na timu ya Kimondo kwani jitihada zote za kujaribu kuondoa aibu uwanja wa
nyumbani kwa Mji Njombe hali iliendelea kuwa ngumu na hadi dakika kumi
zilizoongezwa na mwamzi kumalizika bado Njombe walionekana kuzidiwa pumzi.
Nyongeza ya dakika
ilionekana dhahiri shairi kutaka kusababisha kilio cha bao la pili hivyo mwamzi
akajikuta anapuliza filimbi huku akiangalia huku na kule kuhofia uongozi wa
mkoa uliokuwa upo uwanjani na kushuhudia timu yao ikitoka imetota huku wageni
kutoka Mpakani wakizungumza Kinyiha,Kiwemba,Kinyaki na kinyamwanga huku maneno “Nyinza sana” tununu
fijo”, natemwa, na tukuvifyondomola” yakisikika kwa furaha
Mchezo wa marudiano baina
ya Kimondo SC ya Mbeya na Mji Njombe unatarajiwa kufanyika katika
uwanja wa sokoine mjini Mbeya Jumapili Juni 2 mwaka huu.
Chachandu ya ligi hiyo
inashamihilishwa na namna timu zilivyojipanga kuhakikisha ushindi kwa kufanya
usajiri wa kusugulia meno kwa tupa!!
Nyingine ni Polisi Jamii ya
Bunda mkoani Mara, Biharamulo FC ya Kagera, Saigon FC ya Kigoma na Katavi
Warriors ya Katavi.
Timu zitakazofuzu kucheza
raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati
mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.
May 26, 2013
ZAMBI AFAGILIA JK KUVUNJA BODI YA KAHAWA
Na Danny Tweve Mbozi,
Akizungumza jana kwenye
mkutano wa hadhara ulioambatana na ugawaji
wa madawati kwa shule ya msingi ya Ichenjezya katika mamlaka ya mji wa
Vwawa, Mbunge huyo amesema ingawa hoja hiyo ilionekana kubezwa hatimaye imezaaa
mabadiliko aliyoyafanya mheshimiwa rais kwa kuteua bodi mpya ambayo sasa
itaongozwa na Dr Juma Ngasongwa
Alisema mwaka jana
alimwandikia waziri wa Kilimo Christopher Chiza
kupinga uteuzi uliofanywa na waziri wa Kilimo wakati huo Profesa Jumanne
Maghembe ambapo Dr Eve Hawa Sinare iliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo huku
wajumbe watano wa kamati hiyo wakitokea
mkoa mmoja.
Katika barua yake ya Juni 4, 2012, Mh Zambi pamoja na kumwandikia waziri wa kilimo
pia alinakili barua hiyo kwa Mh Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akielezea
kukiukwa kwa sheria na utungwaji wa kanuni za zao la kahawa bila kuzingatia
taratibu.
Anasema bodi hiyo ya
awali ilikuwa na wajumbe ambao wengine walikuwa na migongano ya kimaslahi na
wengine kutojulikana makundi wanayowakilisha tofauti na bodi ya sasa ambapo
imehusisha wajumbe kutoka maeneo yote ambayo Kahawa inalimwa.
Anaeleza kuwa
anafurahi kusimama mbele ya wananchi kuwa rais amesikiliza kilio hicho na
kuivunja bodi hiyo pamoja na kuiteua bodi nyingine ambayo sasa inahusisha
maeneo yanayozalisha zao hilo.
“ ninafuraha
kuwaelezeni leo hii kuwa tarehe 30 na 31 mwezi huu wadau wa kahawa watakutana
mkoani Morogoro kuzungumzia maendeleo ya zao la Kahawa mkiwa na bodi mpya
ambayo ina uwakilishi niliokuwa naupigania na kuusimamia” alieleza Mh Zambi.
Amesema katika suala
la kutetea maslahi ya wananchi wake yupo tayari kuitwa vyovyote ilimradi
anasimamia ukweli, na kwamba katika hilo kuna wakati alilaumiwa na kuonekana
akitofautiana na waziri aliyeteuliwa na chama chake, na kwamba alifanya hivyo
kwakuwa anatambua kuwa alikuwa akiwakilisha maslahi ya wapiga kura wake na
wazalishaji wa kahawa nchini kote.
Amesema ni vyema pia
wananchi wake wakatafakari kwa makini kauli iliyokuwa ikisisitizwa na Mbunge wa
awali wa jimbo hilo marehemu Halinga kuwa wananchi wa wilaya hiyo wanapaswa
kuwasomesha watoto wao ili kuepuka kuwa chakula cha wasomi.
Alisema neno hilo si
zuri sana kulizungumzia mbele ya jamii lakini ni ukweli kwamba pasipo kusomesha
watoto wao, wataendelea kuwa watumwa wa jamii iliyosoma ambayo ndiyo yenye
fulsa za kufanya maamuzi huku wao wakiwa watekelezaji tu
Akiwa kwenye mkutano
huo uliofanyika nje ya uwanja wa shule
ya msingi ya Ichenjezya Mh Zambi alitoa msaada wa madawati 100 yenye
thamani ya shilingi Milion sita kwa shule ya Ichenjezya na kufikisha idadi ya
madawati 180 ambayo amekwisha yatoa kwa shule hiyo kwa ushirikiano na mamlaka
ya bomba la mafuta TAZAMA.
MWISHO
May 25, 2013
MEELA ASIKIKITISHWA NA HALI YA WANAHABARI MBEYA, ATIA MKONO KUANZISHA SACCOS
MKUU wa wilaya ya Rungwe Bw. Chripin Meela amesema, changamoto zinazokabili sekta ya habari
na vyombo vya habari kwa ujumla ni matokeo ya umuhimu wa taaluma
hiyo katika ukuaji wa demokrasia nchini
Akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa klabu ya wandishi
wa habari mkoa Mbeya unaoendelea ukumbi wa Royal Tughimbe, Mkuu wa wilaya ya
Rungwe Chrispin Meela amesema, wananchi wana matumaini makubwa na vyombo vya
habari na pale kipapota doa la utendaji ni muhimu kujirekebisha kabla ya kutengeza
picha mbaya mbele ya jamii wanayoihudumia
Amesema hali iliyojitokeza hivi karibuni kwenye klabu hiyo
inahitaji kuweka misingi imara ya kiutendaji
na kwamba jitihada za kufanya uchaguzi wakati huu ni hatua muhimu za kuimarisha mfumo
wa kujiwajibisha kama taasisi ya taaluma.
Amesema ikiwa viongozi wa dini na vyombo vya habari
vitajihusisha na ubadhirifu na wizi ni dalili kuwa hakutakuwa na mwingine wa
kukemea jamii itakayokuwa huru na yenye kukemea vita dhidi ya rushwa
Bwana Meela amesema inashangaza kuona hata vyombo vya habari
vinaingia kwenye ufisadi na akaohoji ninani atakayehoji ufisadi serikali na
kwingineko kama nanyi mnaingia kwenye mitego hiyo hiyo?
Katika hatua nyingine amependekeza Vyombo vya habari kujenga utamaduni wa
kujihusisha na ufuatiliaji wa maendeleo vijijini na kwa kufanya hivyo
kutawezesha wananchi kuwasilisha changamoto zinazowakabili kwa watunga sera.
Amesema katika kufikia hilo
ni vyema pia Viongozi wa serikali ngazi za chini kuondoa uoga katika kufanya kazi na vyombo vya habrari na
kwa kufanya hivyo kutasadia kusukuma mbele jitihada za maendeleo
Katika hatua nyingine Bwana Meela amechangia kiasi cha
shilingi 400,000 kwaajili ya uanzishaji wa chama cha kuweka na kukopa cha
wanahabari SACCOS ili kuwezesha kuwapa fulsa wana habari kujisimamia kiuchumi na kupunguza changamoto za kimaisha
zinazowakabili
Katika kufanikisha hilo wanachama wa Mbeya Press club
walijitokeza kuchangishana wenyewe ambapo wamefanikiwa kukusanya mtaji wa papo
kwa papo kiasi cha shilingi 1,400,000/=
Aidha ameshauri klabu ya wandishi wa habari kuwa na ofisi
yake na hvyo kwa kuomba kiwanja kwenye mamlaka za majiji itasaidia kuwapa nguvu
katika kusimamia haki zao wakiwa na uhuru wa kuwekeza kwenye majengo yao.
May 1, 2013
MEI MOSI UWANJA WA SOKOINE, KUMEKUCHA
Uwanja wa Sokoine ambao unakumbukwa kwa hotuba aliyoitoa mwalimu Nyerere Mwaka 1995 ambayo imeendelea kuwa ujumbe wa kila siku kwenye vyombo vya habari hasa kwenye harakati za kusaka madaraka ya kuingia Ikulu
Mpiga picha wa TBC akiwa tayari kwa kazi ya kuleta picha na hatmaye kuunganishwa moja kwa moja kwenye matangazo yanayoendelea kupitia kituo hicho katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya
Wandishi wa habari wakiendelea kufanya kazi zao uwanjani hapo.
Bendi ya Sikinde wakitumbuiza kwenye uwanja wa sokoine wakati wa maadhimisho kabla mhe Rais hajawasili uwanjani hapo kupokea maandamano
Mkuu wa mkoa wa IRINGA Christine Ishengoma akiwasili uwanjani hapo na kusalimiana na timu ya mapokezi
Hapa Mkombe Zanda wa Star Tv akizungumza na mpigapicha katika safu ya mawasiliano Ikulu Fred Maro katika uwanja wa sokoine
aisee Mbeya yetu Mnatisha, picha zenu nimekuwa nikizifuatilia " ndivyo anavyoeleza Fred Maro wakati wakisalimiana na Joseph Mwaisango mwandishi wa Mbeya yetu
Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akisalimiana na mdau Fred Maro kwenye uwanja wa sokoine
Ngoma ya kabila la wasafwa ikiburudisha wakazi watu waliofurika uwanja wa sokoine kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
Timu ya Uhuru Publication ikiwa uwanjani hapo kunadi bidhaa wanazozizalisha ambapo gazeti lao leo lilipata soko uwanjani hapo
Na Timu ya INDABA BLOG
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mkoani Mbeya yameambana na ukaguzi mkali katika milango ya kuingilia ambapo mabango na zana zote zimekuwa kichekiwa kwa vyombo
Hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama uwanjani hapo kwa kuzingatia kuwa ni jukumu muhimu katika kuwezesha nchi kutulia
Imeelezwa kuwa mabango yenye ujumbe wa kejeli yamekuwa yakiishia mikononi mwa maofisa wa idara za usalama na kufanyika screening ya ujumbe unaoingizwa uwanjani
Kwa ujumla uwanja wa sokoine umefurika huku kila kona kukiwa na makundi ya watu wanaotaka kuingia na kushuhudia kupanda ama kimya kwa mishahara na mambo mengine ya wafanyanyakzi ambao kwa namna moja ama nyingine wanaathiri maisha ya kila siku ya ndugu zao
hadi wakati huu saa 5.15 bado kupo shwari na mandamano yanasubiri kiongozi wa nchi Mh Rais Jakaya Kikwete aingie ndipo waendelee na shughuli za kupita mbele ya jukwaa na kukaguliwa
Mpiga picha wa TBC akiwa tayari kwa kazi ya kuleta picha na hatmaye kuunganishwa moja kwa moja kwenye matangazo yanayoendelea kupitia kituo hicho katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya
Wandishi wa habari wakiendelea kufanya kazi zao uwanjani hapo.
Bendi ya Sikinde wakitumbuiza kwenye uwanja wa sokoine wakati wa maadhimisho kabla mhe Rais hajawasili uwanjani hapo kupokea maandamano
Mkuu wa mkoa wa IRINGA Christine Ishengoma akiwasili uwanjani hapo na kusalimiana na timu ya mapokezi
Hapa Mkombe Zanda wa Star Tv akizungumza na mpigapicha katika safu ya mawasiliano Ikulu Fred Maro katika uwanja wa sokoine
aisee Mbeya yetu Mnatisha, picha zenu nimekuwa nikizifuatilia " ndivyo anavyoeleza Fred Maro wakati wakisalimiana na Joseph Mwaisango mwandishi wa Mbeya yetu
Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akisalimiana na mdau Fred Maro kwenye uwanja wa sokoine
Ngoma ya kabila la wasafwa ikiburudisha wakazi watu waliofurika uwanja wa sokoine kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
Timu ya Uhuru Publication ikiwa uwanjani hapo kunadi bidhaa wanazozizalisha ambapo gazeti lao leo lilipata soko uwanjani hapo
Na Timu ya INDABA BLOG
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mkoani Mbeya yameambana na ukaguzi mkali katika milango ya kuingilia ambapo mabango na zana zote zimekuwa kichekiwa kwa vyombo
Hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama uwanjani hapo kwa kuzingatia kuwa ni jukumu muhimu katika kuwezesha nchi kutulia
Imeelezwa kuwa mabango yenye ujumbe wa kejeli yamekuwa yakiishia mikononi mwa maofisa wa idara za usalama na kufanyika screening ya ujumbe unaoingizwa uwanjani
Kwa ujumla uwanja wa sokoine umefurika huku kila kona kukiwa na makundi ya watu wanaotaka kuingia na kushuhudia kupanda ama kimya kwa mishahara na mambo mengine ya wafanyanyakzi ambao kwa namna moja ama nyingine wanaathiri maisha ya kila siku ya ndugu zao
hadi wakati huu saa 5.15 bado kupo shwari na mandamano yanasubiri kiongozi wa nchi Mh Rais Jakaya Kikwete aingie ndipo waendelee na shughuli za kupita mbele ya jukwaa na kukaguliwa