Adverts

Jul 13, 2013

VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO VYAENDELEA KUIANDAMA TANZANIA


Na Anjela Kivavala DSJ

Kila saa mwana mke mmoja amekuwa akifariki dunia kutokana na  matatizo yaujauzito au wakati wa kujifungua imefahamika

Zaidi ya watoto 460 wamekuwa wakipoteza maisha  kila siku 2007 hadi 2008 idadi ya hiyo imepungua hadi  zaidi ya watoto 445 zaidi ya 140 kati yao  walikuwa na umri  chini ya mwezi mmoja  kwa mujibu wa takwimu  zilizo tolewa  wizara ya afya

 Kulingana  na takwimu zilizotolewa na  wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto  hivyo basi kuwekeza katika  huduma ya afya kutaweza kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto

 Ili kupunguza vifo vya mama na mtoto  ni muhimu kuboresha  zahanati na hospitali  hasa vijiji hili kupunguza vifo vya wanawake na watoto vinavyo tokea  nyumbani ambapo  kunakuwa hakuna vifaa vya  kujifungulia

Kupanua uwekezaji katika  huduma zisizo ghali ambazo hunusuru maisha ya mwanamke na mtoto  ikiwa ni pamoja na kutoa  vyandarua  vilivyo wekwa dawa kwa kila familia  hivyo kutapunguza vifo vitokana vyo na malaria

Kuwaelimisha wazazi wote namna ya kuyatibu magonjwa yanayo ua kama vile kuharisha na kutoa chanjo kwa watoto ili kuwa kinga na magonjwa yanayo zuhilika

Hayo yaliandikwa katika ajenda za watoto kila mama lazima awe na fursa ya kujifungua kwa kuhudumiwa na mkunga wa afya hili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

wanaume Mbozi wajitokeza wengi kuondoa mikono ya sweta


Wanaume 4,682 walipata huduma  ya tohara katika wilaya Mbozi katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu imefahamika.

 Hayo yalitolewa katika taarifa ya Mganga mkuu wa wilaya ya mbozi katika taarifa yake katika kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa huduma ya  tohara  kwa wanaume

Wilaya ya Mbozi kabla ya zoezi hilo  ilikadiliwa kuwa ilikuwa chini ya asilimia 60 ikilinganishwa na maeneo mengine

 Kulingana na tafiti zilizofanywa huduma hii ya tohara kwa wanaume imepunguza uwezekano wa wanaume kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi ukilinganisha na wanaume wasiofanyiwa tohara.

 Taarifa ya mganga mkuu wa wilaya ya mbozi inaonyesha mafanikio haya ni sehemu ya mpango wa uhamasishaji jamii uliofanywa kupitia radio na mikutano ya hazara

 Kulingana na taarifa hiyo ina sema mwanaume asiye tahiriwa  anapofanya tendo la ngono kuna uwezekano wa  kupata michubuko kwa hurahisi hambayo ni rahisi  kwa virusi vya ukimwi kupenya kwa urahisi

Aidha unashauriwa kuwa tohara ifanyike  katika mazingira safi na salama pia ifanyike katika jamii kama njia mojawapo  ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Huduma hii ya tohara inashauriwa ifanyike katika hospitali na wataaramu wa afya daktari  au tabibu  kwa usalama ilikupunguza madhara mbalimbali yanayo weza kutokea

Hivyo jamii inapaswa ifahamu kwamba kuna uhusiano  makubwa kati ya tohara nakupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.

 

 

 
Na Anjela Kivavala DSJ

 

Jul 10, 2013

AGHA KHAN YAJITOSA KUOKOA UHAI WA AKINA MAMA NA WATOTO


Na Anjela Kivalala DSJ

Aga khan foundation wakishirikiana na serikali wapo mbioni kutekeleza mradi wa tuunganishe mikono pamoja unaolenga  kuboresha afya ya mama mjamzito na watoto nchini.

Aidha mradi huo unalenga  kuboresha mfumo wa rufaa kwa wagonjwa,kujenga uwezo na huduma za afya kwa mama mjawazito na watoto

 Kulingana na taarifa iliyotolewa na mfuko huo, Mradi huo pia unakusudia kuboresha  kiwango cha upatikanaji wa huduma ya afya kwa mama mjamzito na watoto, kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma ya afya .

Kaulimbiu ya mradi huo wa tuunganishe mikono pamoja  inatafsiriwa kuwa  ‘’hakuna mwanamke ambaye atafariki wakati wa  kujifungua na hakuna sababu yoyote ya  mtoto kufariki kwa magonjwa yanayo zuilika’’. Inafafanua sehemu ya taarifa hiyo

Mpango wa mradi huo wa tuunganishe mikono  pamoja utatekelezwa katika  mikoa mitano  ya  Mwanza Dodoma Iringa Mbeya  na morogoro ili kuboresha afya ya mama mjamzito na watoto.

 Kulingana na taarifa iliyotolewa na  Aga khan health services, utekelezaji wa mradi huo  utafanyika katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia Juni 2013 kwa mikoa mitano nchini Mbeya ikiwa miongoni mwake na wilaya za Mbozi, Kyela na Mbeya zikihusika kikamilifu.

Mradi huo  unafadhiliwa na  shirika la maendeleo la Canada -CIDA  ambapo utekelezaji wake utashirikisha mashirika mengine yakiwemo  AKHST, AKU  na wadau wengine katika jamii huku wizara ya afya na ustawi wa jamii pamoja na Aga Khan Foundation wakiwa wasimamizi wa kuu wa program hiyo.

 

Jul 9, 2013

CHILIPAMWAO WAJITOSA KUWEKA MJI WA TUNDUMA KATIKA HALI YA USAFI



 miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na kikundi cha CHILIPAMWAO katika mji wa Tunduma kuwezesha usafi katika kituo cha afya ambacho kimekuwa kikitoa huduma kwa wakazi wa Tunduma pamoja na watu kutoka upande wa pili wa Mpaka yaani Zambia
Mwenyekiti wa Kikundi cha CHILIPAMWAO  bwana Kulwa Nyondo akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa uongozi wa kituo cha afya  Tunduma, aliyevaa koti la suti ni diwani wa Kata ya Tunduma Mh Frank Mwakajoka

Wanakikundi wa CHILIPAMWAO wakifanya usafi katika mazingira yanayozunguka kituo cha afya cha Tunduma- (Picha zote   na Anjela Kivavala wa dsj)


Na  Angela Kivavala dsj
Halmashauri ya mji mdogo Tunduma imekipongeza kikundi cha wazawa wa mji huo “Chilipamwa” kwa kujitolea katika kufanya usafi katika kituo cha Afya
Diwani wa halmashauri ya mji mdogo Tunduma Ndugu Frank Mwakajoka awapongeza wa zawa  wa mji mdogo kwa kujitolea kusafisha na kufanya usafi katika kituo cha Afya Tunduma
“natoapongezi kwenu kwa kujitolea kwa hali na mali na kwa uzalendo kuupenda mji wenu kwa kujitolea kufanya usafi kwenye kituo chetu cha afya na huu uwe mfano wa kuigwa vikundi vingine” alifafanua bwana Mwakajoka.
Pia aliwaomba  vikundi vingine kuiga mfano kutoka kwa kikundi cha Chilipamwao kwa kujitolea kukisaidia kituo hicho cha afya cha Tunduma pamoja na kushiriki katika shughuli zingine  za maendeleo.
Mwenyekiti wa kikundi hicho cha wazawa wa Tunduma  ndugu Kulwa Nyondo alisema kuwa kipindi kirefu hakuja kuwepo mfumo wa wananchi kujitolea katika shughuri za maendeleo
“tumeamua kujitolea kufanya usafi katika kituo chetu cha afya kwani tumeona usafi au lidhishi na vifaa havikidhi mahitaji katika kituo chetu” alisema bwana Nyondo
Aidha aliwaushukuru uongozi wa kituo cha afya  Tunduma kwa kukubali ombi lao la kujakufanya usafi  katika kituo hicho  na kwamba huo ni mwanzo tu  na kwamba wataendelea kujitolea hata katika shughuli zingine za maendeleo katika mji wa Tunduma
Kikundi hicho cha wazawa kilijitolea vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya 1.5 mililioni ikiwa ni pamoja na kubadili taa katika wadi na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kituo hicho cha afya.

MBOZI YAOMBA KUONGEZA KATA NA VIJIJI VIPYA



Na Angela Kivavala DSJ

Halmashauri ya Wilaya ya mbozi  iko katika mchakato wa kuomba kuongeza kata na vijiji vipya ili kusogeza huduma karibu na wanainchi.

Kata zipatazo sita (6) zinategemewa kuanzishwa  na vijiji 24 baada ya mapendekezo hayo kuwasilishwa ofisi ya Waziri mkuu Tamisemi

Wilaya ya Mbozi ina watu 446,339,Asilimia 88% ya Wakazi wake hujishughulisha na kilimo ambacho huchangia asilimia 80% ya pato la Wilaya.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki katika Maadhimisho ya Siku ya Serikali za Mitaa ambayo hufanyika Julai mosikila mwaka.
Lengo la sherehe hizo ni kutoa mwanya kwa jamii kutambua na kuzifahamu shughuli na huduma mbali mbali zinatolewa na Taasisi za Serikali za Mitaa yaani  halmashauri za Majiji, Manispaa na  wilaya.

ujumbe wa mwaka huu ni “Amani, Uadilifu na Uwajibikaji kwa wote ni Nyenzo muhimu katika mchakato wa Katiba mpya na Ustawi wa Serikali za Mitaa”
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi inaendelea kusimamia utekelezaji wa mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tuko kwenye mchakato wa kupitia Rasimu ya Katiba iliyotolewa kwa kutumia mabaraza ya Kata yaliyochaguliwa yalisomwa katika hotuba kwa wananchi wa mbozi.

Katika kipindi cha mwaka moja uliopita Halmashauri iliajilia wa tumishi wapya 410 kati yao walimu wa sekondari ni 210 na washule za msingi nio 182 na watumishi wa afya ni 10 ambapo kwa kiasi kikubwa ufanisi wa kazi umeongezeka katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa mbozi

Wilaya ina jumlayashule za sekondari 40za selikari ambapo kati ya shule hizo ni shule 1 tu yenye kidato cha tano na sita Halmashauri ya wilaya ya mbozi iko kwenye mchakato wa kuanzisha shule za kidato cha tano na sita katika kata tofauti.

MAJI YAWA KERO TUNDUMA



Na Anjela Kivavala DSJ
Wakazi wa mji  wa Tunduma wamelalamika kutokana na huduma ya maji safi na salaama kuwa kero kubwa kwao.

Maji yamekuwa kero kwa wakazi wa halmashauri ya mji wa tunduma na kero hiyo ina weza kusababisha magonjwa ya mlipuko ikiwemo homa za matumbo na kuhara  kwa wakazi

 Tatizo la kukosekana kwa maji katika mji huo  limekuwa likiongezeka kila siku kutokana naongezeko la watu katika mji huo.

Wakazi wa mji huo wamekuwa wakinunua maji ya kisima kwa bei ya kuanzia shilingi mia mbili hadi mia tano kwa lita ishilini.
 hayo yamesemwa na mkazi wa mji  wa tunduma  bwana Mwafungo wakati akiiomba selikari iwasaidie kutatua tatizo hili la maji  lililo ukumba  mji huo

Mji huo ukiwa na jumla ya visima vipatavyo vinne kati ya visima hivyo ni visima viwili tu vinavyo toa vikiwa havikidhi mahitaji ya wakazi wa mji mzima tatizo hilo linaendelea kuongezeka kufuatia wakazi hao wakijenga katika vyanzo vya maji. 

Tatizo hilo limekuwa likiongezeka siku baada ya siku kutokana na ungezako la watu na makazi  atika mji huo.

AFYA YAPEWA KIPAUMBELE MBOZI



Na Anjela Kivavala DSJ

Wilaya ya mbozi imetoakipaumbele katika  sekta ya afya ikiwa na lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto

Katika sera ya afya ya Tanzania inataka kila kijiji  kuwa na zahanati katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi sera iyo imeweza kuleta matumaini kwa wananchi kujenga zahanati zipatazo 20  kati ya hizo 3 zimekamilika na zimeanza kamilika.

Vifo vya wajawazito na watoto vimepungua kutokana na kuimalishwa kwa huduma za rufaa kuongezeka kwa  wa taaramu na kuongezeka kwa vituo vya huduma ya mama na mtoto ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa vituo vya (RCH) kutoka 30 had 45

Hata hivyo Halmashauri ya wilaya yaMbozi imefanikiwa kuwa navituo vya upimaji wa hiyari wa VVU na vituo vya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kenda kwa mtoto pia halmashauri imefanikiwa  kuwa na vituo 40 vinavyotoa  huduma za kupima malaria kwa kutumia malaria vilivyoboreshwa na kutoa majibu ya uhakika na kwa muda mfupi(Rapid diagnosis Test)

 Halmashauri imefanikiwa kuajili wa fanyakazi katika huduma ya afya wapatao kumi 10 ili kuweza ku kidhi maitaji katika kwa wagonjwa katika wilaya ya mbozi.

Yalisemwa katika  hotuba kwa wananchi wa wilaya ya mbozi katika siku ya selikari za mitaa iliyo fanyika kiwilaya kata ya igamba iliyo andaliwa na ofisi ya mkurugezi mtendaji wilaya ya mbozi ikiwa na kauli mbiu “Amani, Uadilifu na Uwajibikaji kwa wote ni Nyenzo muhimu katika mchakato wa Katiba mpya na Ustawi wa Serikali za Mitaa”