Adverts

Nov 9, 2014

KIMONDO YAWAPIGISHA KWATA WAPIGANAJI WA MLALE JKT, YAWABANJUA 2-1 KWAO



JKT MLALE HOII MBELE YA KIMONDO!!! YAAMBULIA TWO KWA MOJA!!!
Timu ya Kimondo SSC ya Mbozi imeendeleza ubabe tangu irejee nyanda za juu kusini baada ya kuibabua mabao 2-1 Timu ya Masoja ya Mlale Jkt katika uwanja wa majimaji Mjini Songea.

Ikicheza ugenini kwa kujiamini, Kimondo ilijikuta ainakubali kufungwa bao la mapema na kuwaamsha wenyeji Mlale JKT kwa kusherehekea dakika 30 za mwanzo

Kimondo iliamka kwa kasi na kuanza kupeleka mashambuzi kwenye lango la Mlale, ambapo mashambulizi hayo yalidumu kwa muda na kuwapatia bao la kusawazisha.
Kipindi cha Pili mchakamchaka wa Kimondo uliendelea na kuwawezesha kupata bao la pili na hadi mchezo unamalizika wenyeji wameondoka uwanjani wakiuguza maumivu ya kichapo kwenye uwanja wa nyumbani.
kwa mchezo wa leo Kimondo imefikisha pointi 11 ikiwa imeshinda michezo 4 na kufungwa 4 imeshinda magoli 10 na imefungwa mabao 8 ikipanda hadi nafasi ya nne kwenye kundi lao ambalo linaongozwa na timu za Majimaji na Friends Rangers zikifuatiwa na Lipuli na  Kurugenzi
Jumatano Kurugenzi itakuwa mgeni wa Kimondo kwenye uwanja wa CCM Vwawa kujiwinda katika michezo ya lala salama kabla duru la kwanza halijagonga ukingoni.  

Nov 6, 2014

LIGI DARAJA LA KWANZA, KIMONDO KWAO WAMOOOO

Kimondo ya Mbozi imezinduka kwenye uwanja wake wa Nyumbani baada ya kuifanyia mahaba African Sports ya Tanga mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza.

Mchezo huo wa katikati ya wiki ulifanyika uwanja wa CCM  Vwawa, ambapo mchaka mchaka wake ulionekana tangu kuanza kwa mchezo huo ambapo mabao mawili yalipatikana chini ya dakika 20 za kipindi cha kwanza.

Licha ya jitihada za African Sport ya Tanga kuonyesha jitihada binafsi za wachezaji wake, kuna wakati walipotezwa maboya kwa zaidi ya dakika 20 wakizungushwa kwa staili ya haingaisha bwege kutokana na gonga za hapa na pale za Kimondo

African Sport walipata nafasi mbili muhimu ambazo zingewapa ushindi mnono lakini wachezaji wake hawakuwa makini kutupia langoni kutokana na kuwa wazito kama wamefungiwa mawe miguuni.

Hata hivyo Kimondo inapaswa kujilaumu kwa kukosa nafasi nyingi zaidi ambazo zingeweza kubadili ubao wa magoli hata kusomeka 10-0 kama wachezaji wake wangeacha mambo ya "show game" na kurudhika na mabao mawili waliyokuwa wamepata.

Kutokana na matokeo hayo Majimaji ya Songea na Friends Rangers zinagombana kileleni zikiwa na Pointi 15, zikifuatiwa na Lipuli imefikisha pointi 13,Kimondo ikiruka kutoka nafasi ya saba hadi ya tano

Kumekuwepo malalamiko kwa timu wenyeji kutumia viwanja vyao vya nyumbani vibaya, mchezo unaolalamikiwa ni pamoja na Kimondo na Lipuli wiki iliyopita ambapo licha ya Kimondo kufungwa kwa miundombinu, mashabiki wa Iringa waliamua kuhamia Kimondo kuishangilia kutokana na kandanda saafi walillolionyesha licha ya kuminywa!
"Kuna wakati mlinzi wa Lipuli aliudaka mpira ndani ya penarti box, maajabu ya musa mwamuzi aliuchukua mpira kwenye eneo la penalti na kuutoa nje ya 18  hadi mashabiki  wa Lipuli wakaanza kuzomea baada ya makosa hayo kuwa  ya wazi mno!! anaeleza mmoja wa mashabiki walioshuhudia mchezo huo

UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa  Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.
Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.
Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.
Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi. Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.

Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014

RAIS ATEUA MAKATIBU WAKUU NA KUHAMISHA WENGINE

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha mmoja.
            Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa kuwa Makatibu Wakuu ni Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Yohana Budeba ambaye anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Kuhusu uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rais Kikwete amemteua Bw. Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014

Nov 1, 2014

MAKOCHA 35 KUSHIRIKI KOZI YA LESENI C YA CAF





Tanzania Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA

3rd Floor, PPF Tower, Garden Avenue / Ohio Street
P.O.  Box  1574, Dar es  Salaam, Tanzania     .    Telefax:   + 255-22-2861815
E-mail: tanfootball@tff.or.tz     .    Website: www.tff.or.tz








Release No. 168
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 31, 2014
MAKOCHA 35 KUSHIRIKI KOZI YA LESENI C YA CAF
Makocha 35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.

Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia Mchikichini College ambapo washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na vyeti vya kitaaluma vya elimu ya sekondari (academic).

Washiriki wa kozi hiyo ni Abdulmaliki Nemes (Airport FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro Talented Youth Sports Centre), Ally Jangalu (Moro Kids), Amri Saidi (Mwadui FC), Athuman Kambi (Morogoro), Charles Mwakambaya (Burkina Faso FC),  Damian Mussa (Alliance One) na Daudi Sichinga (Kasulu United).

Denis Maneva (Shule ya Msingi Logo), Edgar Juvenary (JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya Msingi Mtimbwilimbwili), Henry Ngondo (Chalinze Academy), Issa Hamisi (Polisi Kilimanjaro), Jumanne Chale (Dar es Salaam), Kizito Mbano (Masasi Alliance), Martin Saanya (Magereza Morogoro) na Masoud Gumbwa (Sokoine University Academy).

Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage Kabange (Kagera Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC), Nsubuga Solomon (Kishoto FC), Nyamtimba Muga (Kizuka Secondary), Oscar Mirambo (Makongo), Rashid Abdallah (Tech Fort Academy), Renatus Shija (Rhino Rangers), Safari Nyerere (Elimu Sports Academy) na Said Lyakuka (Kizuka Stars).

Simeon Mwesa (Mtibwa Sugar U20), Simon Shija (Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu Shooting), Swalehe Allawi Abdul (Alliance Academy), Yasin Bashiri (Kick Off Sports Academy) na Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar).

Wakati huo huo, kutakuwa na kozi ya wiki mbili ya ukocha ya ngazi ya Kati (Intermediate) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 29 mwaka huu.

Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)