Kimondo ya Mbozi imezinduka kwenye uwanja wake wa Nyumbani baada ya kuifanyia mahaba African Sports ya Tanga mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza.
Mchezo huo wa katikati ya wiki ulifanyika uwanja wa CCM Vwawa, ambapo mchaka mchaka wake ulionekana tangu kuanza kwa mchezo huo ambapo mabao mawili yalipatikana chini ya dakika 20 za kipindi cha kwanza.
Licha ya jitihada za African Sport ya Tanga kuonyesha jitihada binafsi za wachezaji wake, kuna wakati walipotezwa maboya kwa zaidi ya dakika 20 wakizungushwa kwa staili ya haingaisha bwege kutokana na gonga za hapa na pale za Kimondo
African Sport walipata nafasi mbili muhimu ambazo zingewapa ushindi mnono lakini wachezaji wake hawakuwa makini kutupia langoni kutokana na kuwa wazito kama wamefungiwa mawe miguuni.
Hata hivyo Kimondo inapaswa kujilaumu kwa kukosa nafasi nyingi zaidi ambazo zingeweza kubadili ubao wa magoli hata kusomeka 10-0 kama wachezaji wake wangeacha mambo ya "show game" na kurudhika na mabao mawili waliyokuwa wamepata.
Kutokana na matokeo hayo Majimaji ya Songea na Friends Rangers zinagombana kileleni zikiwa na Pointi 15, zikifuatiwa na Lipuli imefikisha pointi 13,Kimondo ikiruka kutoka nafasi ya saba hadi ya tano
Kumekuwepo malalamiko kwa timu wenyeji kutumia viwanja vyao vya nyumbani vibaya, mchezo unaolalamikiwa ni pamoja na Kimondo na Lipuli wiki iliyopita ambapo licha ya Kimondo kufungwa kwa miundombinu, mashabiki wa Iringa waliamua kuhamia Kimondo kuishangilia kutokana na kandanda saafi walillolionyesha licha ya kuminywa!
"Kuna wakati mlinzi wa Lipuli aliudaka mpira ndani ya penarti box, maajabu ya musa mwamuzi aliuchukua mpira kwenye eneo la penalti na kuutoa nje ya 18 hadi mashabiki wa Lipuli wakaanza kuzomea baada ya makosa hayo kuwa ya wazi mno!! anaeleza mmoja wa mashabiki walioshuhudia mchezo huo