Adverts

Apr 7, 2009

Kutoka kushoto ni Bwana Saliwe, mmiliki wa hoteli ya high class mjini Tunduma, akifuatiwa na mkewe bi Saliwe, Mkuu wa idara ya Usalama wa taifa wilayani Mbozi bwana Magani, Mwenyekiti wa wenye mahoteli Mkoani Mbeya bwana Vamponji Mahenge, Mkuu wa wilaya Mbozi Bi Halima Kihemba, Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchini Zambia na mpambe wake wakati wa uzinduzi hoteli ya High Class

HOTEL HIGH CLASS TUNDUMA

HII ndo hotel ya HIGH CLASS inayomilikiwa na jamaa mmoja anaitwa Sanga kimsingi tunampongeza mjasiliamali huyu kwa kuupendezesha mji wa Tunduma na kuwa kivutio kwa wageni wanaoingia bongo kutokea upande wa kusini.

ULINZI WA MAKAMPUNI BINAFSI VIPI?

Kampuni za ulinzi zimeongezeka, kila kukicha linaibuka kampuni jipya kweli kazi wanazozifanya haziongezei uhalifu??? hapa ni kikosi kingine kilichozinduliwa wakati wa uzinduzi wa hoteli ya HIGH CLASS TUNDUMA

UJIRANI MWEMA NA ZAMBIA

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bi Halima Kihemba(amehamia Kibaha) akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Nakonde(jina nimemsahau) wakati wa uzinduzi wa hoteli ya mkinga mmoja pale Tunduma HIGH CLASS HOTEL .Hii yote ni katika kuweka masuala ya mahusiano front au siyo

MAZINGIRA MAZURI KVUTIO CHA WAGENI

Usije jilaumu eti wageni hawakutembelei!! fikiria mazingira kama haya kweli wageni watashindwa kumiminika kwako, mikosi mingine mnajitia wenyewe, mtu umejenga bonge la njenge halafu unashindwa kupanda maua wewe vipi???

NAMSHUKURU DOGO ALITUTOA MKOSI

Namshukuru dogo kwa kututoa mkosi ukoo mzima vinginevyo labda tungekufa hakuna aliyenunua gari!!!! ila mmmh gari lenyewe lilikuwa spana mkononi, hivyo hivyo mbele kwa mbele si watasema ukoo wa Tweve wamenunua gari???

WILAYA YA MBOZI INAHITAJI MISAADA ZAIDI

NI Ukweli usiofichika kuwa wilaya ya Mbozi imezidiwa na mzigo wa tatizo la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, hii inatokana na vifo vingi vya UKIMWI miongoni mwa wazazi, jukumu la malezi sasa limetupwa kwa vikongwe, jamani tunahitaji mikono yenu inyoshwe kwa watoto hawa.

ELIMU YA URAIA NI SEHEMU MUHIMU PIA

Mkuu wa shule ya VWAWA wakati huo bwana Mbilinyi akimwaga lugha kwenye mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi(wanafunzi) juu ya kuwepo shirikisho la Afrika mashariki.

KAZI YA KUWEZESHA MAENDELEO VIJIJINI NGUMU

Wataalamu wa shirika la ADP Mbozi wakiwa katika moja ya harakati za uwezeshaji katika kijiji cha MYUNGA, kwa mbali pembeni linaonekana toroli linalosaidia katika harakati za usafirishaji na uchukuzi, hizi ni hatua katika kuleta ufanisi wa kazi vijijini.

MALEZI MAZURI HUANZIA UTOTONI

Jamani nani asingependa mtoto wake apendeze hivi? nafikiri ni jambo la msingi kwa wazazi kuweka kipaumbele kwanza kumpendezesha mtoto, manake tafsiri ya maisha unayoishi wewe na mkeo nyumbani watu huipata kutokana na mwonekano wa mtoto wako!! Hongera rafiki yangu Siwingwa kwa malezi mazuri