Adverts

Nov 30, 2010

PINGAMIZI LA UBUNGE IRINGA MJINI LATINGA MAHAKAMANI


Katibu wa mheshimiwa Monica Mbega bwana Charles Charles akizungumzia pingamizi lililowekwa dhidi ya Mchungaji Msigwa(picha kwa hisani ya francis godwin blog)

MBUNGE wa zamani wa jimbo la Iringa mjini na mkuu wa mkoa wa KIlimanjaro ambaye alikuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Monica Mbega amefungua kesi namba 3 ya mwaka 2010 katika mahakama kuu kanda ya Iringa akipinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea mbunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) mchungaji Peter Msigwa.




Katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Charles Charles alithibitisha mbele ya waandishi wa habari leo ofisini kwake kuhusiana na Mbega kwenda mahakamani kupinga ushindi wa mchungaji Msigwa wa Chadema kwamadai ya kuwepo kwa kasoro zaidi ya 10 zilizopata kujitokeza siku ya uchagua mkuu octoba 31 ikiwemo ya vituo vya kupigia kura kuhamishwa dakika za mwisho na kufanya baadhi ya wapiga kura kutopiga kura.



Kasoro nyingine ni ile ya tofauti ya matoke yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini ambayo kwa mujibu wa Mbega kuwa yalionyesha kutofautiana kwa kura kama 800 na sehemu ila matokeo ya pili yaliyotangzwa bila kuwepo kwa wakala wala mgombea wa CCM yanaonyesha mgombea huyo wa CCM alipitwa kwa kura zaidi ya 2000 na mgombea wa Chadema.



Hivyo alisema kuwa kutokana na kasoro hizo na nyingine nyingi mgombea huyo wa CCM Mbega amelazimika kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo ya uchaguzi mkuu .



Charles alisema kuwa matokeo ya kwanza ya ubunge yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi yalionyesha mgombea wa NCCR-mageuzi Mariam Mwakingwe alikuwa amepata kura 950 na Monica Mbega (CCM) alikuwa amepata kura 16,916 huku mchungaji Msigwa akipata kura 17742 na kuwa matokeo hayo yalitangazwa huku mawakala wa CCM wakiwepo na kupokea hivyo.



Japo baadaye msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo mapya ambayo mgombea wa CCM wala wakala wake hakuwepo ambapo matokeo hayo Msigwa yalimpa ushindi mkubwa Msigwa kwa kupata kura 17,352 wakati Mgombea waNCCR Mageuzi Mwakingwe akipata kura 1292 .



Hivyo alisema kuwa ukitazama matokeo hayo unapata picha halisi ni jinsi gani ambavyo msimamizi wa uchaguzi alivyoshindwa kutoa matokeo sahihi ya jimbo hilo na kuwa hadi sasa mgombea wa CCM hajapata nakala ya matokeo hayo mapya ambayo ndiyo yamempeleka Msigwa bungeni.



Pia alisema kuwa kasoro nyingine ni ile ya idadi ya wapiga kura katika baadhi ya vituo kuonekana kubwa zaidi ya wale waliojiandikisha na sehemu nyingi idadi ya waliopiga kura na wasio piga kura ukijumlisha unakuta kuna tofauti kubwa ya kura kuzidi.



Hata hivyo alishindwa kutaja wakili anayesimamia kesi hiyo kwa madai kuwa atajulikana pindi kesi hiyo itakapoanzwa kusikilizwa pamoja na kujua idadi ya halisi ya kasoro zilizotolewa na Mbega ambaye hakuweza kupatikana kuelezea suala hilo.



Kwa upande wake Mchungaji Msigwa alipoulizwa kuhusiana na madai hayo ya Mbega kwenda Mahakamani kupinga ushindi wake alisema kuwa hata yeye amekuwa akisikia kuwepo kwa suala hilo japo hadi jana alikuwa hajapatakufikishiwa taarifa yoyote rasmi toka mahakamani juu ya kuwepo kwa kesi hiyo.



"Mimi mwenyewe nimekuwa nikisikia kama Mbega amekwenda mahakamani kupinga ushindi wangu ila mimi sijapata taarifa rasmi za kuitwa mahakamani japo ni haki yake ya msingi kwenda mahakamani"alisema Mbunge Msigwa alipoulizwa kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi.



indaba2010

MH MBEGA APELEKA PINGAMIZI MAHAKAMANI KUPINGA USHINDI WA MCHUNGAJI MSIGWA

Taarifa kutoka mtandao wa mdau Francis Godwin unaonyesha kuwa Mh Mama Monica Mbega Mahuvi amefikisha mahakamani pingamizi lake lakutaka matokeo ya uchaguzi wa nafasi ya ubunge kwa jimbo la Iringa mjini yatenguliwe na mahakama kuu

MH Rais anapowafunda mawaziri wake

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana kwa mara ya kwanza na baraza lake jipya la mawaziri ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)


Spika makinda ziarani namibia

Mhe. Anne Makinda (Mb)Spika wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC-PF (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Essau Chiviya , wakati wa kikao cha Kamati Tendaji mjini Swakompmund, Namibia tarehe 29/12/2010 baada ya kupitia agenda na maandalizi ya Mkutano wa 28 wa SADC-PF utakaofunguliwa na Rais wa Namibia Mhe, Hifikepunye Pohamba tarehe

CHILIGATI ANAPOMKABIDHI TIBAIJUKA ILANI

Mh. Chiligati akikabidhi Ilani ya CCM kwa Mh. Tibaijuka ili kutekeleza kwa ukamilifu ahadi za chama hicho kwenye sekta ya Ardhiindaba2010

MASHINDANO YA KUKIMBIZA BAISKELI DODOMA

indaba2010

Makamu wa Rais akutana na Mawaziri wa ofisi yake leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Ofisi yake wakati Mawaziri hao walipokwenda Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo, kwa ajali ya kujitambulisha rasmi. kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dk. Teresya Luoga Hovisa, katikati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe. Samia Hassan Suluhu.indaba2010

ILO; bongo Tunaathiriwa na nchi zinazozotuzunguka zenye maambukizi makubwa ya UKIMWI

Na Danny Tweve


Iringa.



Shirika la kazi duniani tawi la Tanzania limetaja Tanzania kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI kutokana na kupitiwa na barabara kutoka nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi.



Akizungumza kwenye mafunzo ya waelimisharika wa masuala ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika maeneo ya Kazi,



Mratibu wa Mradi wa Kuongeza Uwezo wa kiuchumi na Kupunguza hatari ya Maambukizi kwenye Njia za Usafirishaji kwa chini ya ILO upande wa Tanzania Bi Tulanoga Matimbwi ameeleza hayo jana mjini Iringa wakati akielezea mwelekeo wa mradi huo.

Amesema wakati Tanzania kwa upande wake kiwango cha maambukizi ni 5.7% nchi zinazolisha(feed) barabara kuu ya TANZAM zina maambukizi makubwa hii ikienda sambamba na barabara ya Dar es Salaam hadi Namanga.



Alitolea mfano kuwa nchi zilizo kwenye ukanda wa barabara ya TANZAM hali ya maambukizi ni kubwa kuanzia Zambia ambako kiwango cha maambukizi ni 15.03%,Malawi 14.02%,Zimbabwe 24%,Afrika Kusini 18% Botswana 23.9% na Msumbiji 12%.



Kutokana na hali hiyo amesema ni muhimu kuimarisha jitihada za kukabiliana na maambukizi mapya kwenye vituo vinavyopitiwa na barabara hizo kuu, ili kupunguza madhara ya mwingiliano huo.



Ameainisha kuwa uelimishaji katika mipango yake unalenga zaidi kwenye maeneo ya kazzi katika sekta binafsi na sekta ya umma na kwamba kupitia miundo iliyopo katika ngazi za wilaya itawezesha kufanikisha mapambano hayo.



Mafunzo hayo yanahusisha washiriki kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Dar es Salaam na NJORUMA na wengi wao ni kutoka asasi zinazojengea uwezo vikundi vya kijamii, waratibu wa UKIMWI na maafisa ushirika.

Baada ya dozi hii nawatakia kilalakheri katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe mosi Decemba, Mungu awabairi na kuwajaza nguvu wale wote wanaopata huduma majumbani na wanaopata dawa katika maeneo mbalimbali nchini mwetu na duniani kote. Mchango wenu katika maendeleo ya nchi bado tunautegemea msikate tamaa tupo pamoja nanyi katika kuhakikisha kuwa afya zenu zinaendelea kuimarika kwa kuimarisha huduma za tiba majumbani lakini pia katika kliniki za CTC. ahsante
indaba2010

LUKUVI AKIWA KWENYE OFISI YAKE

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Fanuel Mbonde akiwatambulisha Mawaziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mary Nagu (Mb) anayeshughulikia (Uwekezaji na Uwezeshaji) na Mhe. William Lukuvi (Mb) anayeshughulikia (Sera Uratibu na Bunge) kwa Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizoko chini ya Ofisi hiyo (hawako pichani), tarehe 29 Novemba, 2010 wakati Mawaziri hao waliporipoti Ofisi ya Waziri Mkuu kuanza kazi rasmi baada ya kuapishwa.

MAWAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU WATETA NA WATENDAJI WAO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. William Lukuvi (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Bibi Fatma Mrisho wakati wa mapokezi ya Waziri huyo katika viwanja ya Ofisi ya Waziri Mkuu alipowasili kuanza kazi yake rasmi tarehe 29 Novemba 2010. Nyuma ya Waziri ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Fanuel Mbonde.