Adverts

Oct 25, 2010

CHILEWA AKIFANYA MAJARIBIO KWENYE MOJA YA MAGARI YA TAKA

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Levison Chillewa akijaribu kuwasha moja ya magari yaliyotolewa kusaidia shughuli za usafi katika mji mdogo wa Tunduma ambao upo mpakani mwa Tanzania na Zambia.

MAANDALIZI YA WEKA TUNDUMA SAFI YAANZA

Kampeni kubwa ya kuufanya mji wa Tunduma kuwa safi ikiwa ni harakati za kuiondoa aibu kwenye macho ya nchi jirani kutokana na hali ya uchafu wa mji huo hapo awali- sasa imepamba moto baada ya halmashauri mama ya wilaya ya Mbozi kuamua kuusaidia mji mdogo wa Tunduma magari  mapya mawili ya kuzoa taka yaliyonunuliwa kwa zaidi ya milion 150. Huu ni mfano mzuri kwa miji mingine katika kuhakikisha suala ya la usafi wa mazingira kuwa moja ya maeneo ya kimkakati. Tunduma ingawa ni sehemu ya eneo la wilaua ya Mbozi bado shughuli zake za kiuchumi kwa sehemu kubwa zinachangia mapato ya moja kwa moja kwenye serikali kuu (HAZINA) lakini  wananchi wanahoji kiasi gani kinarejeshwa kwa uhalibifu wa mazingira unaofanywa na shughuli hizo kwenye eneo hilo kwa ujumla? manake maambukizi ya HIV kwa sehemu kubwa yanachangiwa na shughuli hizo za border post  any way tupo kwenye majadiliano karibuni

Christian naye ana matumaini na Tanzania ijayo

Ingawa mama yake anaonekana kama anaelekea kukata tamaa kwa jinsi ninavyoendesha serikali ya familia yangu  lakini kijana wangu Christian anaonekana ana matumaini makubwa na serikali yangu baba yake! Nakutakia maisha marefu na yenye busara na neema mwanangu Christian

Oct 5, 2010

UWANJA WA AMANI ZANZIBAR UPO TAYARI KUTUMIKA

Baada ya ukarabati wa kampuni kutoka China, uwanja wa amani unaonekana murua ukiwa umewekwa zuria kwenye eneo la kukimbilia huku hoteli zake zikiwa saafi baada ya ukarabati mkubwa: picha kwa kudesa kutoka issamichuzi blog

Oct 4, 2010

PM AKIWA NA BAN Ki Moon septemba 27,2010

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana huku akipiga picha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kabla ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za Umoja huo jijiniNew York Septemba 27, 2010. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye umoja wa Mataifa.indaba2010

MAMBO YA FEDE KWENYE MTANDAO WA KATUNI

Mtembelee Mtaalam wa katuni hizi za kisiasa na kijamii na nyanja nyingine muhimu katika 
.BLOG: www.artsfede.blogspot.com.
indaba2010

Morooooooooooooooooooobwana

indaba2010

ETI WANAWAKE HAWABEEP!!! JAMANI WAPENI FULSA

Ujumbe umefika watoto eeeeeeee(indaba2010)

BARUA YA MTOTO KWA MWENYEZI MUNGU

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000
(Laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia.  Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini  hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia  uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi  yake.

Kisha akai-post barua ile.  Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa
ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona  bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.

Barua ilisomeka hivi:
"Mpendwa Mungu,

Jina langu ni EMMANUELEY, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika
jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania ,  bara la Africa .

Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.
Naomba sana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya
kazi na
kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
sana .

Natanguliza shukrani.

Wako mtiifu,
EMMA."


Wafanyakazi wa posta walifurahishwa sana na barua hiyo na kisha wakaamua
waipeleke kwa Rais . Rais  naye alipoipokea ilimfurahisha
sana na
kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani
kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi sana .
Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:
"Mpendwa Mungu wangu,

Nashukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba.
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya Tanzania .Kama ilivyo kawaida yao, wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya kodi , kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu

MAMBO YA MUSTAPHA HASSANALI

 Designers listerning to Patrick Lumumba of the Production Facility they visited on 30 September 2010.
Designers attending how the pattern drafting works

Picha kupitia mtandao wake.