Adverts

Apr 8, 2009

LIPENENGA NGOMA INAYOHAMASISHA AMANI

Vamo vakwijulah naloli, wazee wa kinyaki wakipiga mapenenga kwenye moja ya sherehe mkoani Mbeya. Ngoma hizi ukizifuatilia ni moja ya maeneo muhimu ya kutukumbusha wapi tumetoka wapi tunakwenda na tunakwendaje, kimsingi ni kutokana na matukio ya ngoma kama hizi ndipo uhamasishaji wa masuala ya amani, ushirikiano na upendo vimekuwa vikifanyika bila mwongozo ulio rasmi. Ndiyo sababu wanyaki wanadaiwa kupendeleana sana kwenye post fulani fulani ukweli siyo kwamba wanapendeleana ila wana jali udugu, wazalendo na wapenda mashirikiano.(kwa mujibu wa utafiti-usiniulize ulifanwya wapi na nani). Hebu angalia mzee wa kwanza alivyopiga way kichwani!!!!! hii niliiona moja Dodoma kwenye makuzi yangu haijatokea tena ila Tky unazikuta za kumwaga.