Adverts

Jan 31, 2011

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete awasili Addis Ababa kwa kikao cha Wake wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete awasili Addis Ababa kwa kikao cha Wake wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika: "
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Dr. Jerome Biswaro mara tu alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole huko Addis Ababa tarehe 29.1.2011.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Binti Victoria Madebe huku mtoto mwingine Damian Lubuva akiwa tayari naye kumkabidhi mama Salma shada la maua wakati alipowasiri katika uwanja wa ndege wa Bole huko Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 29.1.2011.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na watoto Victoria Madebe (kushoto), Michael Lyaruu (kulia) na Damian Lubuva (Mwisho), waliofika uwanja wa ndege wa Bole kumpokea. Mama Salma Kikwete yupo Addis Ababa kuhudhuria kikao cha Wake wa wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika kinachoanza tarehe 30.1.11 hadi 31.1.2011.
"