Adverts

Jan 31, 2011

Rais Kikwete kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika

Rais Kikwete kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika: "
Rais Jakaya Kikwete akishiriki katika ufunguzi rasmi wa kikao cha 21 cha Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika jijini Addis Ababa kilichoanza tarehe 30.1.2011.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika ufunguzi rasmi wa kikao cha 21 cha Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika kinachofanyika Addis Ababa tarehe 30.1.2011.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 21 wa Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika huko Addis Ababa tarehe 30.01.2011
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Ghana Mheshimiwa Jerry Rawlings wakati wa kikao cha Marais na Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Afrika kinachofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 30.1.2011.
Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki wakati wa kikao cha Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika kinachofanyika Addis Ababa tarehe 30.1.2011
"