Adverts

May 23, 2011

BRECKING NEWS: DAKTARI AUAWAWA MAKETE KISA MAPENZI!!!

Usiku wa kuamkia jana wanachuo wa Taasisi ya Afya cha Bulongwa Hospitali (Maarufu kama chuo cha Dental na Nursing) wamemvamia, kumpiga, kumjeruhi na hatimaye kumuua daktari wa hospitali ya Bulongwa Dr. Maphingo Jumbe.
Taarifa zilizoufikia mtandao wa indaba africa zinaeleza kuwa Daktari Jumbe amesomea udakatari wa tiba ya binadamu nchini Tanzania MUCHS na baadaye amefanya kazi ya ukufunzi katika masuala ya elimu kwa watumishi wa afya wanaofanya kazi kwenye eneo la VVU na UKIMWI na aliletwa na wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kufuatia upungufu wa madaktari katika hospitali ya Misheni Bulongwa.
Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa ni wivu wa mapenzi. tutazidi kuwaleteeni kadili tunavyopata kutoka makete
Kutoka kwa mdau Jackson Mbogela aliyeko Makete