Adverts

Jan 28, 2013

WAZEE WA NGWASUMA KUFUNIKA SHUGHULI YA KUWAAGA WADAU MBOZI

Kundi la FM academia wazee wa Ngwasuma wanatarajiwa alhamis hii kumwaga mayai kwenye shoo maalumu kwaajili ya kuwaaga wadau wa sekta ya afya wilayani Mbozi walitumikia hadi kufikia mwisho wa utumishi wao kisheria al maarufu wastaafu.

Shughuli hiyo inaambatana na kukaribisha mwaka 2013 ambapo wazee wa Ngwasuma wamekuwa wadau muhimu katika burudani pande hizi hapa za mpakani! na sasa wameamua kuangusha kikosi kizima kwenye shughuli hii

Inaelezwa kuwa wadau kama Brother K kutoka mujini Tunduma na kundi zima la mapedesheee wa boda ni miongoni mwa waliojitokeza kubeba zigo la shughuli hiyo na kwamba burudani ya kufa mtu inatarajiwa kuwekwa katika ukumbi wa Mpemba Makuti Village

Kutokana na kujulikana kwa kundi hilo hadi pande za Zambiatan huko, tayari watu kutoka Nakonde wanaomba wajisogeze kwenye shughuli hiyo hata hivyo kutokana na ukweli kwamba shughuli hiyo haina mtazamo wa kukusanya mapato bali burudani, haitawezekana kubeba abiria nje ya level seat!

Tayari kamati ya maandalizi ya shughuli hiyo ikiongozwa na Godfrey Msokwa imeshakamilisha masuala ya msingi kwa asilimia 99.2 hizo zilizobakia ni za mwenyezi mungu  anaeleza mmoja wa waandaji papa mzee wa migoma!