Adverts

Apr 30, 2009

CHELE BOVU LAMWAGWA!!!!! KWELI NDOMONDO ANATISHA

Jumla ya tani 11 za mchele uliokuwa ukisafirishwa kutoka nchi ya Vietnam kuingia nchini na kukamatwa na Mamlaka ya Mapato nchini, katika mpaka wa Tanzania na Zambia katika mji wa Tunduma wilayani mbozi mkoa wa Mbeya ukivushwa kutokea jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada yan kukataliwa nchini humo, umeteketezwa jana Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa mamlaka hiyo mkoani Mbeya Rogasian Shirima ameeleza kuwa mchele huo ulivushwa katika mpaka wa Tunduma ukipelekwa nchini Kongo Februari 9 mwaka huu ukiwa jumla ya tani 16 ambapo mamlaka ya chakula na afya nchini Kongo iliukataa mchele huo kwa sababu za kiafya na ikaamuru urudishwe Vietnam .Alisema kuwa nchini Kongo walipokea tani 6 tu ambazo zilizokidhi kiwango kwa afya ya binadamu na mwingine kukataliwa ambapo imeelezwa katika nyaraka za usafirishaji wa mchele huo hazikuwa na maelezo ya mzalishaji, mwaka uliozalishwa na tarehe ya mwisho ya kutumika.Naye Afisa Mkaguzi wa Mamlaka ya uthibiti wa chakula na madawa nchini (TFDA) Kalekayo Emmanuel amethibitisha mchele huo kuwa haufai na hivyo kuamuri kuteketezwa ili kuwanusuru wananchi ambao wangeweza kuuziwa chakula hicho.Shehena hiyo ya mchele ilikuwa ikisafirishwa na gari lenye usajili namba T193 AAL na tela T353 AKV aina ya Scania likiendeshwa na dereva Bakari Athuman (51) ambaye ameeleza kuwa alipakia mzigo huo katika bandari ya Dar es Salaam Februari 6 na kuvuka mpaka Tunduma na Nakonde Februari 9 na kwamba amelazimika kukaa Kongo kwa muda wa mwezi mzima baada ya kukataliwa kupakuliwa mzigo huo.Mmiliki wa lori hilo Komuni Sirai amesema kuwa yeye alikodisha gari lake kwa Gabriel Luxo raia wa Kongo ambaye aliingiza mchele huo kutoka Vietnam na kwamba kitendo cha mchele huo kukataliwa kumemfanya apate hasara zaidi ya dola za kimarekani 7000 baada ya mteja wake kutoroka bila kumlipa.Hata hivyo ameshukuru kwa mamlaka hizo kwa kutoa uamuzi ambao umempa nafasi ya kuondoa mchele na kwamba gari lake litaweza kufanya kazi zingine.Baadhi ya watu ambao walishuhudia tukio la uteketezaji wa mchele huo walisema kuwa, kusafirishwa kwa mchele huo kupitia mipaka ya nchi yetu inaonesha kuwa idara zinazohusika na udhibiti wa uingiaji wa bidhaa kutoka nje bado hazijawa makini, hali ambayo imepelekea mzigo huo kufika hadi Kongo na kasha kurejeshwa tena jambo ambalo wamesema linaonesha udhaifu mkubwa.