Adverts

Apr 3, 2009

MADIWANI MBOZI WASUSIA KIKAO

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi jana wamesusia kikao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mkakati wa kuondosha viongozi wake/watendaji. Hoja iliyotolewa na mmoja wa madiwani hao ilieleza kuwa, wamekuwa wakitoa maagizo kwa watendaji bila kupata mrejesho. diwani huyo ajulikanaye kwa jina la Twinzi alitoa hoja iliyoungwa mkono na madiwani wenzake akitaka kikao hicho kivunjwe hadi hapo watendaji watakapoandaa dondoo zote za mihtasari ya kamati zote iliyopita. kikao hicho kimefanywa wakati mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo bwana Chilewa Levison akiwa safarini Morogoro, ambako yeye na wakurugenzi wengine walihudhulia mkutano wa kuhitimisha ziara ya waziri mkuu. Danny Tweve