Adverts

Apr 3, 2009

TIGO YAELEKEZA NGUVU MASHULENI -MBOZI

Mbozi Kampuni ya simu za mkononi ya TIGO imezindua mfuko wa elimu ujulikanao kama TIGO elimu kwa taifa la Tanzania na kukabidhi vitabu 500 vya hisabati kwa shule 10 za sekondari wilayani Mbozi mkoani Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wake. Akikabidhi vitabu hivyo kwa mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh Godfrey Zambi, Meneja wa Tigo kanda ya Kusini bwana Willy Mwakiema amesema chini ya mpango huo, maeneo ya sekta za michezo, afya na hata uchangiaji vifaa vya elimu mashuleni yatazingatiwa ili kuwezesha mazingira bora ya upatikanaji wa elimu kwa watoto. Kwa upande wake bwana Mbunge wa Mbozi Mh Zambi ameelezea kufurahishwa na mpango huo kuzinduliwa kitaifa jimboni kwake na kuelezea hatua hiyo kama Ukombozi kwa watoto walio vijiji hasa kwa kuzingatia mazingira ya shule nyingi zilizo kwenye ngazi ya kata yanafanana, na kukabiliwa na ukosefu wa vitabu husunani somo la hisabati ambalo ni msingi muhimu kwa wasomi wa baadaye. Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo bwana Lingson Ngaikwela na kaimu Katibu Tawala Bwana Salehe Simba wameeleza kuwa matunda ya Mpango wa MEM yanatarajiwa kuanza kuonekana katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka huu na kwamba wilaya ya Mbozi inatarajiwa kufaulisha watoto 13,000 kiwango ambacho nyenzo kama vitabu ni suala la msingi katika kuwaendeleza Makabidhiano hayo yamehudhuliwa na viongozi wa halmashauri ya wilaya na mwakilishi ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na wadau wa elimu wilayani humo ambapo vitabu hivyo kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha tatu vina thamani ya shilingi millionTano Danny