Adverts

Apr 20, 2009

TUFANYE NINI ILI JAMII YA WAFUGAJI ISIWE NA ULE UTARATIBU WA KUHAMA HAMA?

Ndugu wanachama wa blog mbali mbali kwa miongo mingi, makabila ya wafugaji kama wamang'ati, wamasai, Wairaqwi, n.k wamefanyiwa mambo mengi ya kuwalazimisha wabadili mfumo wa maisha yao ya ufugaji wa kuhamahama na usio na tija. Mambo waliyofanyiwa ni kama yafuayo. (i) maeneo yao ya kufugia ya asili kuchukuliwa na selikari either ya kikoloni au ya uhuru na kuyafanya kuwa hifadhi za Taifa. Kwa kufanya hivyo maeneo ya kufugia yalipunguwa sana na kusababisha uhaba wa malisho (ii) Selikari wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni zilihamasisha jamii ya wafugaji kuanza kujishugulisha na kilimo katika maeneo machache yaliyobakia ya kufugia. Ni kweli baadhi ya wafugaji wakaanza kulima katika maeneo ya kufugia. Jambo la kunote hapa ni kuwa, kwa ujumla maeneo mengi ya kufugia sio mazuri kwa kilimo hivyo hupoteza rutuba haraka na kutozalisha chakula cha kutosha. Hivyo hata wale walioamua kulima walilazimika kuendelea kufuga kwa sababu hawakuwa na uhakika wa kupata chakula cha kutosha. (iii) Pale migogoro ya wakulima na wafugaji inapotokea, wafugaji wakati wote wameonekana ndio waanzilishi wa migogoro hiyo linapokuja suala la kuchukuwa hatua tumeshuhudia wafugaji wakifukuzwa, kutozwa faini kubwa, kuporwa mifugo, au kuhamishwa bila maandalizi yoyote. Uhaba wa ardhi katika maeneo yao umesababisha wafugaji wengi kuhamia katika maeneo mengine na kujikuta katika migongano na jamii nyingine. Na migogoro inapotokea, tunawasikia baadhi ya viongozi na wenyeji wa maeneo husika wakiwataka warudi walikotoka. Njia hizi za kutatua matatizo ya wafugazi zimekuwa si endelevi kwa ustawi wa jamii za wafugaji na maendeleo ya watanzania kwa ujumla. Je wanaJF nini kifanyike ili kuboresha maisha ya wafugaji? Kama Botswana waliweza sisi ni kitu gani kimetuzuia? Tunapojadili hili, tukumbuke kuwa Tanzania ina ardhi tele ambayo inafaa kwa kilimo na kufugia mpaka tunataka kuwagawia wageni hekta 500,000. Na wengine tayari wameshajichukulia ardhi katika bonde la mto rufiji na kwenye vijiji ya Kisarawe Pia tukumbuke kuwa baadhi ya maeneo hayafai kwa kilimo cha mazao bali kwa ajili ya kufugia tu. Karibuni tujadili