salam za OB kwa JK
Rais wa Marekani,Barrack Obama
Kwa niaba ya Marekani, Ninawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha uchaguzi mkuu hivi karibuni na kuendeleza utamaduni wenu wa kuendesha chaguzi za vyama vingi toka mwaka 1992.
Ninatarajia kufanya kazi na Rais Jakaya Kikwete na wabunge wa Bunge la Kumi tunapoendelea kujenga na kuimarisha ubia wa muda mrefu na wenye mafanikio kati ya mataifa yetu katika kuendeleza malengo ya pamoja ya maendeleo na kukabiliana na changamoto nyingi za kimataifa zinazotukabili.
Aidha, ninatoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad, serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa na zaidi sana kwa watu wa Zanzibar ambao wameweka historia kwa kufanya uchaguzi wa amani baada ya miaka kadhaa ya chaguzi zilizogubikwa na machafuko.
Kama nilivyomueleza Rais Kikwete nilipokutana naye katika Ikulu ya White House hapo mwaka 2009, Watu wa Marekani wanawaunga mkono Watanzania wote katika jitihada zenu za kuimarisha utawala wa kidemokrasia na uwazi, kutumia kikamilifu fursa za Muungano wenu na kuhakikisha kuwa hatua mlizopiga na mafanikio mliofikia katika kujenga amani na ustawi wa kudumu hayarudi nyuma.