Adverts

Jan 31, 2011

BREAKINGNES ...MAPIGANO MAKALI IRINGA YAUA MMOJA

BREAKINGNES ...MAPIGANO MAKALI IRINGA YAUA MMOJA: "

MAPIGANO makali ya kugombea eneo la kunyweshea mifugo yaibuka katika kijiji cha Pawaga wilaya ya Iringa vijijini kati ya wafugaji jamii ya kimasai na wasukuma na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyeuwawa kwa kukatwa katwa mapanga huku kijana aliyetambuliwa kwa jina Merick Vanihi kujeruhiwa vibaya kwa mshale katika mkono wake wa kulia. Wakielezea juu ya tukio hilo mashuhuda walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa chanzo cha mauwaji ya ni wafugaji jamii ya wasukuma ambao wamekuwa na kawaida ya kulazimisha wakulima kukubali mashamba yao yatumike kama sehemu ya malisho ya mifugo yao. Imeelezwa kuwa eneo hilo yalipotokea mapingano hayo kuna dimbwi la maji ambalo limetokana na mvua zinazoendelea kunyesha na jirani wamekuwa wakiishi wafugaji jamii ya kimasai ambao pia wamekuwa wakiendesha kilimo katika eneo hilo . Hivyo siku ya tukio wafugaji jamii ya kisukuma walifika katika eneo hilo na kulazimisha kunywesha maji mifugo yao pamoja na kulisha mifugo mazao ya wenyeji wa eneo hilo jamii ya kimsai kwa kutumia nguvu zaidi hali ambayo iliibua ugomvi mkubwa kati ya pande hizo mbili. Kutokana na nguvu zaidi zilizotumiwa na jamii ya wafugaji wa kisukuma ,wafugaji jamii ya kimasai pia walilazimika kuingilia kati ili kusaidia wenzao na kupelekea ugomvi huo kuwa mkubwa na kuwafanya wasukua kutumia silaha kali kujinusuri zaidi. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha kutokea mauwaji hayo kuwa yametokea juzi majira ya saa 7 mchana na kumtaja mfugaji jamii ya kimasai aliyeuwawa katika mapigano hayo kuwa ni kijana Iyani Kalihi (24). Kamanda Mangalla alisema kuwa kijana huyo aliuwawa kwa kuchomwa katika sehemu mbali mbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali . Aliwataja watu wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo Machia Bachilo (54) Msukuma ,Kimbemba Bachilo (56),Sandu Magosi(28),Tewe Bundara(30),Zachalia Sanga (34) Hata hivyo alisema kuwa majeruhi huyo amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa akiendelea kupatiwa matibabu zaidi kutokana na mapigano hayo..

"