Jan 15, 2011
DUKA LAFANYA PROMOTION KWA KUDHALILISHA WATU NCHINI HISPANIA
DUKA LAFANYA PROMOTION KWA KUDHALILISHA WATU NCHINI HISPANIA: "Wakiwa wamevaa nusu uchi mamia ya wakazi wa jiji la Madrid nchini Hispania walivumilia baridi kali na kupanga foleni kwa masaa kadhaa mbele ya duka ambalo lilikuwa likitoa nguo za bure kwa watu waliovaa nusu uchi.
Zaidi ya watu 200 wakiwa wamevaa nusu uchi walipanga foleni mbele ya duka ambalo lilikuwa lilitoa ofa ya nguo za bure kwa watu waliovaa vichupi tu.
'Njoo ukiwa umevaa nusu uchi na uondoke ukiwa umevaa nguo za bure', ndio maneno yaliyoandikwa kwenye matangazo ya duka la Desigual la mjini Madrid ambalo lilikuwa likipromoti bidhaa zake na kuanza msimu mpya wa mapunguzo ya bei katika msimu wa baridi.
Wanawake wakiwa wamevalia vichupi na sidiria tu huku wanaume wakiwa wamevaa chupi tu, walipanga foleni mbele ya duka hilo kwa masaa zaidi ya 12 wakisubiria nguo za bure.
Duka hilo lilitangaza kutoa nguo za bure kwa watu 100 wa kwanza kuingia ndani ya duka hilo wakiwa wamevaa nusu uchi.
Watu waliofanikiwa kuingia ndani ya duka hilo walijichagulia nguo mbili za bure na kuzivaa ndani ya duka hilo na kutoka bila ya kulipa chochote. "
new post