Jan 29, 2011
Egypt Moto Bado Unawaka: Hosni Mubarak Avunja Baraza La Mawaziri
Egypt Moto Bado Unawaka: Hosni Mubarak Avunja Baraza La Mawaziri: "
Hatimaye Rais Hosni Mubarak ameongea na watu wake.
Ametamka kuwa amevunja baraza la Mawairi. Lakini yeye atabaki kama Rais. Leo ataunda Serikali mpya itakayotoa suluhu ya matatizo ya WaMisri.
Obama ameongea na Hosni Mubarak na kumtaka atimize aliyoyasema. Na kwamba arudishe mawasiliano ya simu na internet kwa watu wake. Obama katoa tamko pia: ' Tuko pamoja na watu wa Misri'.
Siku za Hosni Mubarak Ikulu huenda zinahesabika. Mwenyewe anapima upepo, na kuna wengine wengi wenye kufanya hivyo.
Egypt na Hosni Mubarak ni mshirika mkubwa wa Marekani. Ni kiungo muhimu cha Marekani na Dunia ya Waarabu.
Marekani inaweka taadhari kubwa. Itataka kuwa na hakika ya nani atachukua nafasi ya Hosni.
Mohamed ElBaradei anaweza kuwa chaguo kubalika kwa Marekani. Lakini, kama akikataliwa na Muslim Brotherhoods wakajikita kuziba hombwe ni nini kitatokea? Kuna maswali yanayotakiwa majibu yake na Marekani.
Na Hosni Mubaraka hajaelewa, kuwa wanachotaka WaMisri wengi kwa sasa sasa si Serikali mpya inayoongozwa na Mubarak. Kwa WaMisri , miaka yake 31 Ikulu imetosha. Na chama chake nacho kimepoteza mvuto.
Ndio, Egypt ni taifa kubwa katika Arab World. Akianguka Hosni Mubarak, basi kuna wengine wengi katika Dunia ya Waarabu, ambao, himaya zao zitaporomoka kama nyumba ya karata. Siku chache zijazo zitaamua mustakabali wa Dunia ya Waarabu na watu wake.
Na Tusubiri tuone.
Maggid
Iringa."