Adverts

Jan 13, 2011

“ESTA”-SKYWALKER Ft SALIMO

“ESTA”-SKYWALKER Ft SALIMO: "

Nilishawahi kusema kwamba miongoni mwa mambo ninayoyapenda hapa BC ni pamoja na fursa ya kuwatambulisha wasanii chipukizi,producers,actors,actresses,comedians, nk.Kwa miaka kadhaa ambayo BC imekuwa hewani,jambo hilo bila shaka tumelifanya kwa upana wa aina yake.

Leo naomba kumtambulisha kwenu Fredrick Bundala au kwa jina la kisanii Skywalker. Huyu yawezekana asiwe mgeni sana kwa baadhi ya watu hususani wasikilizaji wa radio kwani yeye ni mtangazaji wa kituo cha Radio Free Africa kitu ambacho kwa njia moja ama nyingine tayari kinamuweka karibu na masikio ya wengi.

Mbali na utangazaji,Skywalker ni msanii na pia ni producer.Na kwa wimbo ambao utausikiliza hivi punde,naweza kumuingiza katika kundi la “uanaharakati”.Katika wimbo huu ambao ameupa jina la Esta, Skywalker anazungumzia kisa cha mtoto wa mtaani.Ni kisa cha kutunga lakini kinachoakisi maisha ya ukweli.

Nini huwa kinatokea mpaka mtoto anaishia mitaani na kubatizwa jina la “mtoto wa mtaani”?Ok…kuna wale wanaoondokewa na wazazi wote na kutokuwa na ndugu yeyote wa kujitolea kuwalea.Mambo yanapokuwa hivyo,wengine huamua kuishia mitaani.

Lakini unajua kwamba kuna watoto wengi tu ambao hukimbia nyumbani na kuishia mitaani kwa sababu mtaani kuna “nafuu” kuliko nyumbani?Jamii ina nafasi gani katika hilo?Usikilize wimbo wa Esta hapo chini.Producer wa wimbo huu ni mwenyewe Skywalker na hapa amemshirikisha msanii Salimo.

" indaba2010