Balozi wa Zinduka Profesa Jay,   akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi  wa habari Dar es Salaam jana  kuhusu Tamasha la Tuzo za wasanii wa mziki  wa Injili linalotarajiwa  kufanyika februali 27 Kulia ni Mratibu wa  Tamasha hilo, Haris Kapiga.
TANZANIA   Gospel Promoters (TGMP) kwa mara nyingine tena baada ya miaka mitano   kupita wameandaa tamasha la Tunzo za Muziki wa Injili (Gospel Music   Awards) lililopangwa kufanyika Februari 27 katika Ukumbi wa Diamond   Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo asubuhi  katika   mkutano na waandishi wa habari Mratibu wa Tamsha hilo Haris Kapinga   kutoka Kampuni ya Clouds Media Haris Kapinga alisema tamasha hilo   litatumika kuwapongeza na kufanya tathmini ya jumla kwa wasanii binafsi   na tasnia nzima huku Tunzo mbalimbali zitatolewa.
Tunzo hizo ni  wimbo  bora wa mwaka, mwandishi bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kike wa  mwaka,  mwimbaji bora wa mwaka wa kiume, kundi bora, msanii bora wa  muiziki wa  Injili wa mwaka na mwimbaji anayechipukia katika uimbaji wa  nyimbo za  Injili.
Wimbo wa mwaka, video bora, Mtayarishishaji bora  wa mziki wa  video wa mwaka , Mtayarishaji bora wa muziki, Tunzo ya  Jumuiya, Kwaya  bora ya Akapela,Kwaya bora inayotumia ala, bendi bora ya  muziki wa  Injili, Kwaya bora inayotumia ala ya Piano.
“Jinsi watu  watakavyoweza  kupiga kura, kura zitaanza kupigwa Januari 29 mwaka huu  na kufikia  kilele cha February 12 huku fomu zote zilizopigiwa kura  zitatakusanywa  Februari 13” alisema Kapinga.
Anaendelea kwa kusema  kuwa mdhamini  mkuu wa tamasha hilo ni Mradi wa kutokomeza Malaria ,  Zinduka ambao  zaidi ya lengo kuu la kupambana na Malaria inatumia  tamasha hili  kuwaunganisha viongozi wa dini mbalimbali kwa kuanza na  madhehebu ya  dini ya Kikristo ili kupeleka ujumbe kuhusiana na  mapambano dhidi ya  ugonjwa wa Malaria.
Tangu Mradi huo ulipoasisiwa  nchini mwaka 2010  umekuwamradi wa kwanza unaofanya kazi kwa  kushirikiana na sekta  mbalimbali katika jamii ili kusimamia pamoja na  kumaliza ugonjwa wa  Malaria nchini kote.
Mkutano huo ulihudhuriwa na  viongozi wa dini  ambao ni Sister Mariana Francis kutoka Roman  Catholic, Mchungaji David  Mwasota ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Makanisa  ya Kipentekoste, Mchungaji  Solomon na John Gao wa Makanisa ya  Anglican, ambao wote kwa pamoja  wamewakumbusha wana jamii na kuwahimiza  Watanzania katika kujilinda,  kuepukana na vifo vinavyoweza kuzuilika.
“Tunaimani  kwamba kwa  kutumia nguvu ya muziki wa Injili , mwamko na ufahamu  kwenye jamii  vitaongezeka sana huku jamii na waumini wakiunganisha  nguvu ya kupambana  na Malaria” alisema Mwasota. 
 

