Anatoka katika familia iliyoshika dini.In fact,Baba yake ni Mchungaji Peter Sanga wa kanisa la Haven of Peace Church la jijini Dar-es-salaam.Yeye ni mtoto wa tatu kuzaliwa kutoka kwenye familia ya Mchungaji Sanga.
Kama ilivyo kwa wanamuziki wengi,alianza kuimba kanisani akiongoza watoto wenzake katika shule ya Jumapili au Sunday School.Alikuwa na umri wa miaka 9. Hivi sasa ana umri wa miaka 20.Kutoka katika shule ya jumapili,akajiunga na kwaya ya wakubwa ya kanisa. Ikawa nafasi nyingine kwake kuonyesha na kuthibitisha kipaji alichonacho katika uimbaji.
Hapo ndipo alipoonwa na Marehemu Dr.Remmy Ongala ambaye alimualika kuimba katika kwaya yake na baadaye ndipo Linah aliporekodi wimbo wake wa kwanza wa Injili uliokwenda kwa jina Nimekukimbilia.
Ilikuwaje akatoka kanisani na kuingia alipo hivi sasa? Ilikuwa hivi; Clouds FM walikuwa wanaendesha “kashindano” ka kuimba.Kama mtu anajisikia anajua kuimba,basi anapiga simu na kupewa dakika moja ya kuimba na kisha wasikilizaji wanapiga simu na kuchagua mshindi. Linah alifanya hivyo na kuwemo katika washindi Kumi waliochaguliwa kupitia zoezi hilo.
Huo ndio ukawa mwanzo wa Linah kufika Tanzania House of Talent (THT) na hatimaye hapo alipo hivi sasa ambapo majuzi wakati THT inatimiza miaka 5,alikuwemo miongoni mwa wasanii kutoka THT waliozindua albums zao.Ya kwake inaitwa Atatamani.
Mbali na muziki pia Linah pia ni muigizaji kwani kwa sasa amesaini mkataba wa na clouds Tv ambako ataonekana katika tamthilia inayokwenda kwa jina la ’69 Records’ ambayo itakuwa inarushwa na Clouds Tv.
"