Adverts

Jan 31, 2011

madereva taxi na bodaboda wapewa somo na jeshi la polisi mkoani kagera

madereva taxi na bodaboda wapewa somo na jeshi la polisi mkoani kagera: "
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Kagera, Marson Mwakyoma (mwenye shati la drafti) akiwapa somo waendesha magari yanayobeba abiria wakati akitoa elimu kwa madereva kwa njia ya vitendo iliyotolewa na kikosi hicho jana kwa kushirikiana na Chuo cha Lake Zone kwenye viwanja vya Gymkana vilivyoko katika manispaa ya Bukoba, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Udereva cha Lake Zone, Winston Kabantega na kulia kwake ni PC Mwinyi mkaguzi wa magari.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Kagera, Marson Mwakyoma akitoa elimu kwa njia ya vitendo kwa waendesha pikipiki zinazobeba abiria katika manispaa ya Bukoba, kushoto kwake ni Mkaguzi wa Magari wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Kagera, PC Alexander na mwenye suti ni Mkurugenzi wa Chuo cha Udereva cha Lake Zone, Wiston Kabantega, elimu hiyo ilitolewa kwenye viwanja vya Gymkana, elimu hiyo ni sehemu ya mikakati ya jeshi la polisi Mkoani Kagera ya kupambana na ajali mkoani Kagera.
"