Adverts

Jan 21, 2011

Mama Rahma Al - Kharous atoa msaada wa sh. mil 30 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti

Mama Rahma Al - Kharous atoa msaada wa sh. mil 30 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti: "
Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd ,Mama Rahma Al Kharous akizungumza na wanahabari leo juu ya udhamini wake wa shilingi mil. 30 kwa ajili ya ukarabati wa msikiti wa Al - Auwariyya uliopo eneo la Gongoni,Bagamoyo.
Unavyoonekana msikiti huo hivi sasa kwa upande wa mbele,ambao ndio msikiti wa kwanza kujengwa katika mji wa Bagamoya ukiachana na ile iliopo kule Kaole.Msikiti huu ulijengwa mwaka 1889 na kuufanya kuwa ni moja ya sehemu za historia katika mji huo.
Sehemu ya nyuma ambayo imeshaanza kuanguka kutokana na kukaa kwa siku nyingi.
Mama Rahma Al-Kharous (katikati) akiwa na viongozi wa msikiti ambao ni Sheikh Abdul Rahman Bura (pili kushoto) na Mweka hazina wa Msikiti huo,Sheikh Mohamed Shariff (pili kulia) pamoja na kijana aliekuwapo msikitini hapo.
Mama Rahma Al - Kharous (katikati) akiwa na baadhi ya ndugu zake alioongozana nao leo kwenda kuuona msikiti huo.toka kushoto ni Mama Rahma Ibrahim,Sharifa Ismail,Amina Kasiga pamoja na watoto wao.
"