Athumani Mussa (Mwalubadu) anakuja na komedi kali na fupi inayokwenda kwa jina la Rafiki (Friend in Salon), 
“Ninataka kuwaonyesha raia kuwa kazi naweza hata peke yangu  ndiyo  maana nimemua kucheza komedi fupi yenye maana na inakwenda ZIFF kuonyeshwa huko katika tamasha kubwa zaidi mwezi  wa saba, lengo langu kwa sasa ni kuwa muigizaji wa kimataifa”
Mwalubadu amesema kuwa anatarajia komedi hii kuwa ni tofauti kabisa na komedi ambazo amekuwa akionekana  kwa sababu nyingi huwa hatungi yeye bali ushirikishwa tu lakini hii mtunzi ni mwenyewe, 
Ntafanyia huku huku  Iringa  kwa mara ya kwanza natolea mzigo huku.
