SAKATA la Studio aliyotoa Rais Jakaya Kikwete limechukua sura mpya baada ya Mbunge wa Mbeya mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Joseph Mbilinyi kudai kuwa anashangazwa na tamko lililotolewa na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kuhusu studio hiyo ambayo Wizara imedai kuwa ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete kufuatia ombi binafsi la Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Tanzania House of Talent (THT).
Mbilinyi ukipenda unamuita Mr Two au Sugu alisema yupo tayari kula kiapo kuhakikisha haki inatendeka katika suala hilo na atalifikisha bungeni kwa kuwa tamko la Wizara limelenga kulinda watu wachache, walionufaika na mamilioni yaliyotolewa na Rais Kikwete kwa ajili ya wasanii huku wakiwakandamiza wasanii ambao ni walengwa.
Kauli ya mheshimiwa Sugu imekuja siku mbili baada ya Wazira ya Habari Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi kutoa tamko mwishoni mwa wiki ikieleza kuwa Studio iliyotolewa na Rais ni ombi binafsi la THT, ambalo ilimuomba rais wakati alipohudhuria sherehe zao za kutimiza miaka mitatu Desemba 8 mwaka 2008…
Endelea kusoma habari hii kupitia Mwananchi
" new post