Adverts

Jan 31, 2011

Milango iko wazi ubalozini Dc- Mh.Mwanaidi Sinare Maajar

Milango iko wazi ubalozini Dc- Mh.Mwanaidi Sinare Maajar: "

Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akitoa hotuba yake mbele ya watanzania waishio Washington Dc metro area.

Pamoja na mambo mengine alitoa nafasi ya watanzania hao kuweza kwenda kumwona ofisini kwake kila Jumanne na kufanikisha uchaguzi wa kamati ya katiba ya jumuiya ya watanzania.

Aidha mh. Balozi pia aliwapa nafasi maafisa wake wa ubalozi kujitambulisha kwa watanzania na pia kutoa mawasiliano yao wazi ikiwemo simu na barua pepe na kuweka bayana kuwa milango ya mawasiliano kati ya ubalozi na watanzania iko wazi. Balozi pia alikuwa wa kwanza kutoa mawasiliano yake wazi mbele ya watanzania wa Washington Dc ikiwemo mpaka nambari yake ya mkononi kitu ambacho hakijawahi kuonekana kwa viongozi wengine waliopita katika ofisi yake.

"