Miss Progress International, Julieth Lugembe akifuta machozi mara baada ya kulia kutokana na simulizi ya kusikitisha aliyoipata kutoka kwa mtoto Dorcus Meela.
Miss Progress International, Julieth Lugembe akimsikiliza mtoto Dorcus Meela aliyemfanya aangue kilio kutokana na mambo aliyokumbana nayo kutokana na hali yake ya ulemavu wa ngozi.
Mtoto Fatma akimbusu Julieth alipotembelea shule kwao. Fatma alisema anataka kushiriki shindano la Miss Progress akiwa mkubwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Peter Mwendapole pamoja na Miss Progress Intenational wakiwa wamekaa na watoto Flora na Fatuma ambao walisema wanataka kushiriki shindano la Miss Progress wakiwa wakubwa
Miss Progress International, Julieth William Lugembe akimvalisha mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi kofia zilizotolewa msaada. Watoto hao wanaosoma katika shule ya Mukidoma Arusha
NA JONTHAN TITO.
MISS Progress International, Julieth William Lugembe, jana aliangua kilio wakati alipotembelea shule ya sekondari Mukidoma wakati alipokutanma na watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule hiyo.
Julieth ambaye yuko kwenye ziara ya kujua matatizo wanayokabiliana nayo alibino, alishindwa kujizuia kulia baada ya mmoja wa wasichana wanaosoma sekondari kueleza matatizo yake yanayomfanya ashindwe kusoma vizuri.
Msichana huyo Dorcus Meela ambaye yuko kidato cha tatu katika shule huyo alisema yeye alifiwa na wazazi wake wote wawili na hana msaada wowote hali ambayo inafanya asipate mahitaji yake muhimu.
Alisema ndugu wamemtenga kwa kuwa yeye ni mlemavu wa ngozi na kutoka na tatizo la ngozi yake hawezi kufanya vibarua ambavyo vingeweza kumpatia kipato ili apate pesa ya matatizo.
Mwingine Maria Charles huku akieleza kuwa mama yake ni mchuuzi katika soko kuu la Moshi, mkoani Kilimanjaro.
'Mi huwa nalazimika kuvuta kurudi shule, mama yangu anafanya kazi ambayo haiwezi kunipatia mahitaji muhimu, nakosa viatu, nakosa madaftari, baba yangu aliondoka tangu nilipozaliwa naishi kwa kusaidiwa tu na watu, kama hapa sina viatu,' alishindwa kuendelea kuongea na kuangua kilio kilichopokelewa na mrembo huyo wa dunia nja kufanya ofisi ya mwalimu mkuu kupatwa na ukimya kwa muda.
Katika shule hiyo pia wanafunzi wengine walisema wazazi wao wengi waliwakimbia baada ya kuzaliwa na hata wale waliopo hawana uwezo wa kuwasomesha ingawa walishukuru uongozi wa Makidoma kwa kugharamia masomo yao.
Ziara ya Julieth imeratibiwa na kampuni ya One Touch Solutions inayoandaa shindano la Miss Progress Tanzania, na kudhaminiwa na shirika la ndege la Precision Air pamoja na kampuni ya simu ya Airtel na hoteli ya Corridor Springs Arusha.
Matatizo yaliyoelezwa katika mazungumzo hayo ni pamoja na kukosekana kwa magodoro ya kulalia, vyandarua, madaftari, sabuni ambapo ilielezwa Empirial na Dettol zinawasaidia kwa ajili ya ngozi zao pamoja na lensi kwa ajili ya kusomea.
Akijibu kauli zao, Julieth aliahidi kusaidia upatikani wa mahitaji hayo na kuahidi kurejea tena shuleni hapo ili kuona nini kitakuwa kimepatikana.
'Kwakeli inanisikitisha lakini nawataka msikate tamaa tutasaidia kuhakikisha tunapunguza haya matatizo hata kama si kumaliza kabisa lakini naahidi kurudi tena hapa mwezi ujao kuona nini ambacho ninaweza kutatua,' alisema.
Awali alionana na watoto wa shule ya msingi ambao wengi wao walionekana kukosa sare za kanisani, vitabu, madaftari pamoja na magodoro na vyandarua.
Julieth yuko katika ziara ya kutambua matatizo yanayowakabili watu na wototo wenye ulemavu wa ngozi kabla ya kuwapelekea msaada sahihi. Alipokuwa Shinyanga katika kituo cha Buhangija, mrembo huyo alikutana watoto wanalala watatu watatu katika kitanda kimoja chenye ukubwa wa futi mbili na nusu hali ambayo ni hatari kwa afya zao.
Watoto hao mbali ya kuomba magodoro na vitanda pia waliomba kupatiwa televisheni ili waweze kujua yanayoendelea dunia. Pia waliomba kupatiwa madaftari na vitabu vya shule ya msingi.
"