Adverts

Jan 28, 2011

MKUU WA WILAYA MBOZI AWAPIGA MADONGO WANAOZAA OVYO

Na Danny Tweve Mbozi

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo amesema uzazi wa mfululizo hadi mbegu ziishe siyo ushujaa na badala yake ni kuandaa watumwa na mikokoteni katika siku zijazo.
Akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya shule ya sekondari ya Wiza iliyopo wilayani humo inayomilikiwa na Unyiha Associate, amesema tofauti na miaka iliyopita wakati ambapo elimu ya Kidato cha nne ilionekana zna thamani, baadaye ikafuatiwa na elimu ya Kidato cha sita kuonekana ya thamani hali ya sasa imebadilika ambapo mtu bila shahada ya kwanza ni bure.
Amesema hakubaliani na utaratibu wa wazazi kuendelea kuzaa pasipo kujua  namna watakavyowasomesha watoto hao kwakuwa kuzfanya hivyo ni kuwaandaa kuwa watumwa wa wenzao.
,Maneno hayo yameonekana kuwaingia sawa sawa wazazi wengi katika mahafali hayo ambapo alieleza wazi kuwa wakati serikali ikihangaika na idadi ya sasa ya watanzania ni dalili kuwa hali itakuwa mbaya huko mbele ambapo tayari ushindani na nchi jirani unazidi kuimarika.
Aidha amezungumzia suala la wahitimu kujiandaa na changamoto za maisha ya utu uzima kwa kuzingatia kuwa wanakwenda kwenye jamii za ushindani.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Unyiha Associate Bwana Charles Chenza amesema matokeo ya kidato cha nne ni changamoto kwa wazazi kusimamia nidhamu ya watoto na kuwaandaa vyema na kwamba katika hatua za kukabili ushindani shule hiyo imeanza kutoa scholarship kwa watoto wanaomaliza darasa la saba waliofaulu vizuri kusomeshwa bure.\
Amesema tayari kuna wanafunzi wawili wanaufaika na mpango huo na kwamba katika awamu ijayo uongozi unaangalia uwezekano wa kuongeza nafasi hizo ili kuchukua wanafunzi wenye ushindaji.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyoPeter Oichi amesema matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2010 yanaonekana kuwa mabaya kutokana na shule hiyo kurithi wanafunzi wa shule ya awali ya Joseph baada ya kuuzwa kwa kampuni hiyo.
Alisema tofauti hiyo inajitokeza kutokana na tofauti kubwa katika matokeo ya kidato cha pili mwaka huu ambapo shule hiyoimeshika nafasi ya 17 katika shule 350 za kanda ya nyanda za juu kusini na kwamba kutokana na changamoto hiyo ya matokeo, uongozi wa shule unalenga kuimarisha zaidi suala la kuchuja wanafunzi bora kujiunga na shule hiyo.
Katika mahafali hayo walimu waliofanya maajabu wamezawadiwa ambapo mwalimu wa kike mwenye diploma alionyesha kufanzya vizuri katika somo lake la civics amzbapo shule hiyo ilishika nafasi ya saba katika matokeo ya  kidato cha pili mwaka huu.
mwisho