Adverts

Jan 31, 2011

Neno La Leo: Dowans; Kuku Anayekimbia Na Panzi Mdomoni!

Neno La Leo: Dowans; Kuku Anayekimbia Na Panzi Mdomoni!: " Ndugu Zangu, HUTOKEA, kuku akimdaka panzi mdomoni, basi, ukimwandama ukimpigia kelele. Kuku huyo atakimbia na panzi wake mdomoni . Mara ile atakapoona umesitisha kumfukuza , na kelele pia. Basi, kuku huyo, taratibu ataanza kumla panzi wake. Lakini, kama utaendelea kumwandama na kumpigia kelele, hutokea, kwa kuku anayekimbia na panzi mdomoni, kumtema panzi ili kuandamwa huko kwishe. Dowans ni kama kuku na panzi wake mdomoni. Alishamdaka, kabla hajaanza kumla, Watanzania tumeamka na kuanza kumwandama Dowans huku tukimpigia kelele. Kuku Dowans ameonyesha dalili za kuweweseka. Tukiongeza kupiga kelele, basi, upo uwezekano wa Dowans kumtema panzi. Naam. Tuendelee tu kupiga kelele za ’ HATULIPI!, HATULIPI! ’- NON SI PAGA! Kwa Kiitalia. Yumkini panzi aliyemdomoni mwa Dowans anaweza kutemwa! Itakuwa nafuu kwetu. Na Hilo Ni Neno La Leo. Maggid Iringa, Jumatatu, Januari 31, 2011 mjengwa
"