Ilikuwa furaha ya aina yake kwa watu na wadau wa blog hii kijijini kushuhudia mwaka 2010 ukikata kauli na kuingia 2011 katika ukumbi wa Shimoni Village! Mtaalamu wa kilimo kwanza wilaya ya Mbozi akisikilizia maelekezo kutoka high table
Watu walikuwa Nyomi ama kwa kiswahili tulichozoea kwetu kijijini watu walikuwa wengi kwenye part hii kama ambavyo unaweza kushuhudia hata dada Mage na mama Chomoka walikuwemo pia
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Levison Chilewa alikuwa hana makuu kwenye shughuli hiyo na badala yake alikuwa ametulizana kushuhudia kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha 2011
DSO Mbozi bwana Msangi alikuwa akitafakari namna ya kuanza 2011 kwa yale majukumu ya kumsaidia Rais pembeni akiwa amepozi katibu tawala wilaya ya Mbozi bwana Magacha