Msanii anaekuja kwa kasi katika anga ya muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva aitwaye Sam akiwatumbuiza wakazi wa Tunduma na wimbo wake wa Sina raha jioni ya leo kwenye uwanja wa mwaka.
Pichani ni wasanii Mwasiti pamoja na Quick Racka wakilishambulia jukwaa mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Tunduma jioni ya leo kwenye tamasha la Msimu wa raha kamili na serengeti
Baadhi ya wakazi wa mji wa Tunduma,Mkoani Mbeya wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Msimu wa raha kamili na Serengeti lililofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Mwaka.Tamasha hilo lilipambwa na wasanii kibao akiwemo Linux,Amin,Barnaba,Lina,Quickracka,Godzilla,Mwasiti,Ditto,Beka Boy na wengineo,Tamasha hilo litafanyika kesho mchana kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Sokoine kwa kiiingilio cha shilingi 1,000/= kwa kila kichwa.picha zaidi bofya hapa
"