Halmashauri ya wilaya ya Mbozi katika jitihada zake za kuweka mpangilio wa miji ya Tunduma, Vwawa na Mlowo, jitihada za ugawaji viwanja zinaendelea hivi sasa kwa miji hiyo.
Kwa mujibu wa afisa ardhi wilaya hiyo, kuna uwezekano wa kuunganisha mji wa Vwawa na Mlowo wakati pia eneo la Mpemba limo kwenye hatua za kuunganika na Tunduma baada ya viwanja kugawanywa kwenye eneo la Chapwa.
Viwanja vya packing na miradi mikubwa ni sehemu mojawapo iliyotengwa katika eneo la chapwa na kwamba serikali inatarajia kujenga makazi ya watuumishi wa mamlaka ya mapato TANZANIA ambao wamo kwenye mpango wa kuunganisha kituo kimoja cha kuota huduma baina ya Zambia na Tanzania.
Kwa sasa maombi ya viwanja yanapokelewa na idara ya ardhi kwaajili ya maeneo ya Mpemba, Old Vwawa na Vwawa yenyewe.
Aidha ujenzi katika eneo la mpakani unaonekana kuanza kuwapa hofu wengi kutokana na watu wengi kuwekeza majengo ya thamani hasa mahoteli, super market na upanuzi wa miradi ya viwanda vya mazao ya kilimo.
Aidha kwa upande wa kuelekea sumbawanga tayari mashamba ya pembezoni mwa barabara hiyo yamepanda thamani kutoka bei za awali za shilingi 20,000 kwa ekari hadi kufikia 100,000/= kwa ekari.