Adverts

Jan 19, 2011

Wawekezaji Mgodi wa Makaa ya Mawe wakutana na Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal kushoto, akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Sichuan Hongda kutoka China inayotaka kuwekeza mradi wa Makaa wa Mawe na Chuma katika Vijiji vya Liganga na Mchuchuma Wilayani Ludewa Mkoani Iringa, wakati Ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Liu Canglong ulikwenda Ofisini kwa Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo kwa ajili ya Mazungumzo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Sichuan Hongda kutoka China inayotaka kuwekeza Mradi wa Makaa ya Mawe na Chuma katika Vijiji vijiji vya Liganga na Mchuchuma Wilayani Ludewa Mkoani Iringa Bw. Liu Canglong katikati, akimkabidhi Zawadi Maalum Makamu wa Rais Mhe.Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati Ujumbe wa Kampuni hiyo Ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa Rais Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Sichuan Hongda kutoka China inayotaka kuwekeza Mradi wa Mkaa wa Mawe na Mkaa wa Chuma katika Vijiji vya Liganga na Mchuchuma Wilayani Ludewa Mkoani Iringa, wakati Ujumbe huo Ulioongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Liu Canglong, ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo kwa ajili ya Mazungumzo.
"