Adverts

Feb 7, 2011

Al-shabaab Kufungua Idhaa Ya Matangazo

Al-shabaab Kufungua Idhaa Ya Matangazo: " Kundi la kiislamu la Al-Shabab ambalo linadhibiti eneo kubwa nchini Somalia litaanza kurusha matangazo kupitia mitabendi ya kawaida Katika taarifa waliyotoa kupitia kituo cha televisheni cha ya Al-Kataib, Al-Shabaab limesema kuwa video ilyooneshwa kwenye televisheni ilikuwa ya jasusi kutoka ng'ambo aliyekamatwa nchini Somalia. Al Shabaab imewahi kupiga marufuku matangazo kupitia televisheni na redio katika maeneo inayodhibiti na kudai kuwa hayafuati maadili ya kiislamu. Waandishi wa habari wanasema kuwa watu wachache Mogadishiu wana televisheni zinaoweza kupata matangazo ya Al-Shabaab. Al_Kataib wamekuwa wakirusha matangazo kati ya saa kumi na mbili unusu jioni na saa nne usiku, saa za Mogadishu. Idhaa hiyo inatangaza kwa kisomali. Pia kuna matangazo kwa lugha za kiarabu na kiswahili, pamoja na maelezo kwa kisomali na kiingereza. Idhaa hiyo hufungua mfululizo wa vipindi kwa kwa kusoma sura za Kuran, kufuatiwa na hotuba za viongozi wa Al-Qaidah kama vile Usamah Bin Laden, Ayman Al-Zawahiri na viongozi wengine wa kiisalmau. Al-Kataib pia imekuwa ikionesha mahojiano na makamanda kutoka Al-shabaab wakiongea kuhusu Jihad. Sura za wasimulizi na wanaohojiwa zitakuwa zimefichwa. Kulingana na taarifa zilizotolewa na BBC monitoring, baadhi za habari kutoka Al-Kataib zilionesha watu waliodai kuwa raia wa Kenya, Pakistan na Sudan wakidai kuwa wamo nchini Somalia kujiunga na Jihad.
"