Adverts

Feb 27, 2011

BIASHARA NI MATANGAZO NA NI KUTANGAZA KWA STAILI TOFAUTI.

Kijana Mohamed Rashid Mkazi wa Kigamboni akiwa ameshikilia mizani yake ambayo anaitumia katika biashara yake ya kupima uzito kwa malipo ya shilingi mia moja kwa kila mtu anayepima uzito. Mohamed anasema biashara hii angalau inamsaidia kiasi katika kujikimu kimaisha uilinaganisha na biasahara yake aliyokuwa akiifanya mwanzo ambapo alikuwa akiuza mayai ya kuchemsha, anasema kwa siku moja anaweza kupata kiasi cha shilingi kuanzia elfu tatu mpaka elfu kumi kutegemea na biashara ya siku hiyo. Hata hivyo ameongeza kwamba analazimika kulipa shilingi elfu mbili kila siku kwakuwa mizani hiyo amekodishwa hivyo kwa sasa anajitahidi kukusanya fedha ili aweze kununua mizani ya kwake ambayo anaamini inaweza kumuongezea kipato zaidi ukilinganisha na sasa hivi.
"