Adverts

Feb 14, 2011

Born Again Pagan: Tanzania, Na Indonesia: Mwanzo Karibu Mmoja; Mafanikio Tofauti – Hitimisho

Born Again Pagan: Tanzania, Na Indonesia: Mwanzo Karibu Mmoja; Mafanikio Tofauti – Hitimisho: " Msomaji, makala zangu mbili zilizopita (kuhusu vigezo au viungo vya ukwamuzi wa nchi za Indonesia, Malaysia na Singapore, kwa ujumla) zilijaribu kujenga taswira ya kuzielewa nchi hizo. Huenda, zimekusaidia kubaini tofauti zilizopo kati ya nchi hizo na Tanzania yetu. Hii ni makala ya tatu (na ya mwisho) kuhusu nchi za Asia Mashariki na ya Mbali. Madumuni yake ni kuangalia vigezo au viungo tulivyoona (katika makala yangu yaliyopita) na kujaribu kuvivalisha juu ya Singapore ili tuweze kubaini kwa u-karibu kwa nini imefanikiwa kujikwamua kutoka dimbwi la umasikini na kuiacha Tanzania yetu nyuma na hali zilijitawala wakati mmoja na zote zilikuwa zinalingana kwa umasikini. Cha maana mbele yetu si kurudufisha mifano ya Indonesia, Malaysia na Singapore kwa Tanzania, ambayo mazingira yake ni tofauti na hizo nchi. Kujikwamua kwa Tanzania kunaweza kuwa ni tofauti, pia. Hata hivyo, tunaweza kujifunza baadhi ya vigezo vichache na “very eclectically” na ‘pragmatically’ kuzingatia vilivyo ‘constructive’ kwa mustakabali wa Tanzania – jukumu la makala zitakazofuata. Unaposoma utabaini kuwa ninachanganya majina mawili kwa makusudi tu: Kisiwa cha Singapore (kabla ya uhuru) na Singapore (baada ya uhuru). Kisiwa Kidogo Singapore (The City of Lions) ipo kwenye Ukanda wa Joto wa Ikweta wenye joto na ufukutu mkali. Sehemu hiyo iko ki-mkakati (strategically) kwa usafiri wa majini kwenye Mlangobahari wa Malacca kutoka na kuingia Bahari ya Hindi, Bahari ya China Kusini, Bara la Australasia (Asia ya Mbali, Australia na New Zealand) na ni uwanja wa ndege mkubwa kwa usafiri wa angani. Singapore, ‘chunusi kwenye uso wa Malaysia’, ... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com
"