Adverts

Feb 1, 2011

BRECKING NEWS MAJAMBAZI YAFUNGA BARABARA NZEGA

Watu wanaosafiri kwenda mwanza na mikoa mingine kupitia barabara ya Nzega leo usiku  wamekumbana na unyama wa kuvuliwa nguo na kuporwa kila kitu huku magari yaoyakivunjwa viooo.
Taarifa kutoka eneo la Tukio zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wakati magari yaliyokkuwa yakipeleka msiba kwa mbali kuona majabali yakiwa barabarani, hivyo kushtuka fasta fasta.
Inaelezwa na mmoja wa waliokuwa kwenye safari hiyo waligeuza gari lakini wakati wakigeuza alitokeza jambazi mmoja ambaye alikuwa karibu nagari na kujaribu kuzuia lakini akashindwa na kujitosa porini baada ya kuhisi angezidiwa nguvu kutokana na ujasiri wa dereva.
Kutokana na hali hiyo walitoa taarifa polisi, lakini inadaiwa polisi NZEGA walichukua zaidi ya Dakika 45 kuji-organise na hatimaye kwenda eneo la tukio ambako walikuta  magari mengi yakiwa yametekwa na watu kuvuliwa nguo huku uharibifu mkubwa ukiwa umefanywa kwenye magari hayo.