Adverts

Feb 28, 2011

chadema wamtembelea mama maria nyerere butiama

Mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati viongozi na baadhi ya wabunge wa chama hicho, walipomtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama Jumapili hii.
Mama Maria Nyerere akiteta jambo na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, wakati viongozi wa Chama hicho na baadhi ya wabunge, walipomtembelea nyumbani kwake Butiama.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salamu za chama hicho kwa Familia ya Mwalimu Nyerere, wakati vongozi mbali mbali na wabunge wa chama hicho, walipomtembela Mama Maria Nyerere (katikati) nyumbani kwake Butiama. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa.Picha zote na mdau Joseph Senga.
"