Adverts

Feb 25, 2011

HASHEEM THABEET AJIUNGA NA HOUSTON ROCKETS!

Mtandao wa timu ya Basketball ya Houston Rockets toka Marekani (mji ambao unasemekana kuwa una raia wa-TZ wengi)....jana jioni ulitangaza kuwa Mtanzania Hasheem Thabeet anayechezea ligi ya NBA nchini Marekani amejiunga na timu yao toka Memphis Grizzlies ya mjini Memphis-Tennessee kwa makubaliano maalum ya kubadilishana wachezaji.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo wachezaji wawili wa Houston Rockets wamejiunga na Memphis Grizzlies ambao ni Shane Batier (Forward/Guard) na Ishamel Smith (Guard) na mchezaji toka Yugoslavia,Goran Dragic toka timu ya Phoenix Suns ya Arizona pia amejiunga na Houston Rockets.

Hasheem hucheza kama Center na mchezaji wa nafasi hiyo kwa sasa wa timu ya Houston Rockets,Mchina Yao Ming (urefu wa futi 7 na inch 6) ni mgonjwa kwa sasa hivyo iliwabidi watafute faster ngongoti mingine wa kuziba nafasi yake.

"